Mary Masanja Alivyoshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

Mary Masanja Alivyoshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
NW UTALII MHE. MARY MASANJA ALIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja ameshiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza Machi 8, 2023.

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mhe. Mary Masanja alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongoza vizuri Taifa la Tanzania na pia kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha masuala yote ya Utalii na Uhifadhi kupitia programu ya “Royal Tour”.

Mhe. Mary Masanja akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima ametumia fursa hiyo kukabidhi Vifaa vya Watoto Njiti kama Vitanda, Mashine za Oxygen, Mirija na Vifaa mbalimbali alivyovipata kutoka kwa Taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa lengo la kuokoa maisha ya mtoto Njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba.

Aidha, Mhe. Mary Masanja ametumia fursa hiyo kugawa Mitungi ya Gesi ya ORYX kwa kinamama wajawazito ili waweze kuepukana na changamoto ya kutafuta nishati ya kuni za kupikia na badala yake watunze mimba zao ili watoto wazaliwe wakiwa salama.

KAULI MBIU: "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu Katika Kuleta Usawa wa Kijinsia"
WhatsApp Image 2023-03-10 at 13.04.00.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-10 at 13.04.01(3).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-10 at 13.04.01(1).jpeg
 
Back
Top Bottom