Masaa 24 biashara Kariakoo, hali ya usalama mitaani wanakotoka wateja inaruhusu?

Masaa 24 biashara Kariakoo, hali ya usalama mitaani wanakotoka wateja inaruhusu?

Mambo ya siasa tu haya, ila hakuna ukweli wowote
Nani atafungua duka lake na kuajiri wafanyakazi zaidi ili auze 24/7
Nimpe fisi bucha eti

Na huyo wa kutembea na hela akafanye manunuzi saa 6 ya usiku anajielewa ?
 
Hata sasa kuna watu wanatoka usiku mkubwa kwenda masokoni kununua bidhaa,,,,machinjioni n.k.....
kwa hiyo faida ni nyingi kuliko hasara.....hatuwezi kuacha kufanya kazi kwa kuogopa wahalifu...dawa ni kupambana nao.
Na kutakuwepo shift hasa kwa wale machinga wanaomwaga bidhaa chini shift ya kwanza inaanza saa 1 asubhi mpaka saa1 jioni na nyingine inaanza saa 1 jioni mpaka kesho asubhi hivyo hivyo mpaka mwaka unaisha, vijana wasio na ajira ni wengi na hawezi kupata nafasi ya kuuzia bidhaa yao.
 
Zakem si wanauza nyanyachungu na dagaa mchele tu, kibaka nani atakupora fugu la bamia? Saa tano usiku ni muda wa kawaida dar lakini sio saa 9 usiku. Hebu ajaribu kwenda kisha urudi kwenu mtaa wa mnyamani na TV Yako moya uone kitakachokupata.
Hujielewi, kariakoo kuna watu wengi kutoka mikoani wananunua vitu hapo, unapakiza kwenye gari, a siku hizi watu hawatembei na cash, unalipa online kwa lipa namba, shida iko wapi?
 
Itatusaidia sisi wa mikoani naweza nikafika daa sa nane usiku nikaingia dukan bt usalama hapo ndio shida
 
Mbona hii imekuwa issue sana wakati wanywaji hatujawahi kupewa hii attention ilhali tumeanza siku nyingi kupata huduma 24 hrs?
Ama kweli elimu yetu Iko chini sana. Eti mtu anashindwa kutofautisha kati ya mlevi aliyechunwa pesa zake zote bar na madadapoa bar na mtu aliyebeba box la tv ya inch 56 aliyonunua kariakoo usiku wa manane. unadhani vibaka hawana akili kama wewe.
 
kavulata/ kabeberu
 
Hivi ni mtaa upi dar uko salama hata usiku wa manane?

Tunadandia treni kwa mbele. Biashara 24 hours lazima kuwa na supporting background. Yaani lazima mitaa na barabara zote kusiwe na Giza na kufungwa kamera za ulinzi na anuani za makazi ziwe vizuri kabisa, vinginevyo ni maafa matupu na vilio mitaani.
watz tuko na shida sana, kama unaona usalama mtaani kwako ni mdogo nyakat za usiku, nenda mchana, usiku waachie wengine, kwani umelazimishwa kwenda kkoo usiku wa manane.kwani
 
Hivi ni mtaa upi dar uko salama hata usiku wa manane?

Tunadandia treni kwa mbele. Biashara 24 hours lazima kuwa supporting background. Yaani lazima mitaa na barabara zote kusiwe na Giza na kufungwa kamera za ulinzi na anuani za makazi ziwe vizuri kabisa.
discussion postponed by this point
 
Mambo ya siasa tu haya, ila hakuna ukweli wowote
Nani atafungua duka lake na kuajiri wafanyakazi zaidi ili auze 24/7
Nimpe fisi bucha eti

Na huyo wa kutembea na hela akafanye manunuzi saa 6 ya usiku anajielewa ?
Eti nitoke tandale niende kariakoo nikanunue simu ya touch saa sita usiku, najipenda?
 
Eti nitoke tandale niende kariakoo nikanunue simu ya touch saa sita usiku, najipenda?
Hawa wanasiasa wanaongea utumbo wakati mwingine
Wana lao jambo
Camera zinawekwa halafu utasikia hazifanyi kazi tena
Kumbe lilikuwa dili
Yaani waajiri watu wa kuangalia camera 24/7
Wakati waizi wa mitandaoni wanashindwa
 
Ni jambo zuri kufanya biashara masaa 24 na Serikali inachopaswa kuhakikisha ni Usalama watu wake ndani na nje ya kariakoo.

Sidhani kama serikali itashindwa kwenye hilo cha muhimu ni kuinga mkono serikali.
 
Back
Top Bottom