TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Utalii ni sehemu mojawapo inayoingizia mapato nchi yetu na sekta hii ikiwa imetia ajira nyingi kwa watanzania na kuruhusu wageni wengi kuja na kuwekeza mamilioni ya fedha hapa nchini, hali inayofanya mapato kupitia sekta hii kuwa imara kutokana na mambo mbalimbali.
Mpaka ninapoandikaada hii ni masaa zaidi ya 36 tangu moto ulioanza kuwaka kwenye mlima Kilimanjaro, na miali yake bado inaendelea kuenea pamoja na kikosi cha zimamoto na watu mbalimbali wanaojitolea kwa nguvu zote kwenda kupambana na moto ambao uko mita 2800 juu ya usawa wa bahari.
Chuo kinachotoa mafunzo ya utalii na usimamizi wa mali asili cha mwika pia kimewataja wanafunzi wote waliopo chuoni hapo kuingia kwenye uwanja wa mapambano ili kuongeza nguvu kuuzima moto huo ambao umeharibu ekari kadhaa za mimea ya asili inayopatikana eneo hilo, na kufikia juzi majira ya saa 09:00 kulikuwa na watu zaidi ya 400 wakishirikiana na vikosi vya zimamoto wakiendelea kuzima moto huo.
☝️Picha ilipigwa usiku wa siku ya kwanza.
☝️Picha ya mapema juzi iliyopigwa kutokea eneo la himo.
#save_mount_kilimanjaro