Masaa 48, Mlima Kilimanjaro bado ukiwa unateketea

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Utalii ni sehemu mojawapo inayoingizia mapato nchi yetu na sekta hii ikiwa imetia ajira nyingi kwa watanzania na kuruhusu wageni wengi kuja na kuwekeza mamilioni ya fedha hapa nchini, hali inayofanya mapato kupitia sekta hii kuwa imara kutokana na mambo mbalimbali.

Mpaka ninapoandikaada hii ni masaa zaidi ya 36 tangu moto ulioanza kuwaka kwenye mlima Kilimanjaro, na miali yake bado inaendelea kuenea pamoja na kikosi cha zimamoto na watu mbalimbali wanaojitolea kwa nguvu zote kwenda kupambana na moto ambao uko mita 2800 juu ya usawa wa bahari.

Chuo kinachotoa mafunzo ya utalii na usimamizi wa mali asili cha mwika pia kimewataja wanafunzi wote waliopo chuoni hapo kuingia kwenye uwanja wa mapambano ili kuongeza nguvu kuuzima moto huo ambao umeharibu ekari kadhaa za mimea ya asili inayopatikana eneo hilo, na kufikia juzi majira ya saa 09:00 kulikuwa na watu zaidi ya 400 wakishirikiana na vikosi vya zimamoto wakiendelea kuzima moto huo.

IMG_20201012_124054.jpg

☝️Picha ilipigwa usiku wa siku ya kwanza.

Kili.jpg

☝️Picha ya mapema juzi iliyopigwa kutokea eneo la himo.

#save_mount_kilimanjaro
 
Mimi niko moshi mjini ila nauona vizuri kabisa moto huo ambao upo zaidi ya kilometa 60 kutoka hapa nilipo. Kwakweli inaelekea moto ni mkubwa kuliko taarifa zinavyosema. Jitihads za ziada zinahitajika kuuzima
 
Mlima hauteketei,

Msitu unao uzunguka mlima Kilimanjaro ndio ulishika moto na kusambaa kwa kasi, lakini umezimwa tayari.

[emoji110][emoji1241]
 
Huwezi kuutenganisha msitu wa mlima na mlima wenyewe. Msitu unaozunguka mlima Kilimanjaro ni sehemu ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Unapopanda mlima Kilimanjaro unapita katika ya huo msitu. Na mpaka jana Usiku mamlaka za Tanzania zimekuwa zikisisitiza kuwa juhudi za kuuzima ule moto bado zinaendelea (hivyo moto ulikuwepo)
 
Utalii ni sehemu mojawapo inayoingizia mapato nchi yetu na sekta hii ikiwa imetia ajira nyingi kwa watanzania na kuruhusu wageni wengi kuja na kuwekeza mamilioni ya fedha hapa nchini, hali inayofanya mapato kupitia sekta hii kuwa imara kutokana na mambo mbalimbali.

Mpaka ninapoandikaada hii ni masaa zaidi ya 36 tangu moto ulioanza kuwaka kwenye mlima Kilimanjaro, na miali yake bado inaendelea kuenea pamoja na kikosi cha zimamoto na watu mbalimbali wanaojitolea kwa nguvu zote kwenda kupambana na moto ambao uko mita 2800 juu ya usawa wa bahari.

Chuo kinachotoa mafunzo ya utalii na usimamizi wa mali asili cha mwika pia kimewataja wanafunzi wote waliopo chuoni hapo kuingia kwenye uwanja wa mapambano ili kuongeza nguvu kuuzima moto huo ambao umeharibu ekari kadhaa za mimea ya asili inayopatikana eneo hilo, na kufikia juzi majira ya saa 09:00 kulikuwa na watu zaidi ya 400 wakishirikiana na vikosi vya zimamoto wakiendelea kuzima moto huo.

View attachment 1600117
☝️Picha ilipigwa usiku wa siku ya kwanza.

View attachment 1600116
☝️Picha ya mapema juzi iliyopigwa kutokea eneo la himo.

#save_mount_kilimanjaro
Jana magazetini wamesema helikopta itatumika kujua chanzo cha moto huo ambacho mpaka sasa hakijajulikana. Hapo ikumbukwe mjuaji JPM alishangaa sana Andengenye alipotaka kununua drones, akasema zina kazi gani kwenye kuzima moto.
 
Moto ukizima watalii watakuja kwa wingi kutoa rambi rambi kwa kivutio icho, ukishazima zifanyike juhudi kuutangaza mlima na wahamasishe wazungu waje kupanda miti kwa kulipia kuhakiksha nao wanakua katka sehemu ya #Nature_recover or #getwell_soon our nature,
 
Back
Top Bottom