Masaada: ushauri wa haraka

Masaada: ushauri wa haraka

Rahajipe

Senior Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
165
Reaction score
63
Wana JF Salaam.
Leo nakuja nikihitaji kupata ushauri wenu wa kitabibu.
Kwa sasa nina matatizo ya kiafya yanayonisumbua;
Kwanza kabisa kabla ya yote naomba nitoe background yangu ili iwe rahisi kupata picha ya matatizo yangu. Nina tatizo la vidonda vya tumbo, nilikuwa nakunywa bia kwa wingi na sasa nina karibia mwaka tangu nimeacha kabisa kunywa, napenda sana maharage, nakula pilipili sana, kwa ujumla sichagui chakula.
Sasa tatizo kubwa ambalo naona linazidi kushika kasi hivi sasa, tumbo langu linakuwa linaunguruma na kujikuta nikijamba sana karibia kila baada ya dakika chache japo mishuzi mingine haitoi halufu.
Lakini jambo lingine nimejikuta nikiwa siwezi kula aina yoyote ile ya matunda, na pindi ninapojaribu kula hutapika papo hapo, aidha hata nikiangalia tu mtu akiwa anakula najisikia kichefuchefu!
Hata upatikanaji wa choo si mzuri kwa sasa.
Je, tatizo ni nini na nifanyeje? Ikibidi ni PM jamani.
Mods naomba japo liwepo front kwa muda ili nipate ushauri.
 
Avatar yako inaweza kuwatisha wasitoe ushauri mzuri, au madakitari walishazoe kuyaona yote.

Any way subiri watakuja wakimaliza majukumu, ila pole pia
 
pole sana kamanda ucjali tumia maji mengi hata litre 3 kwa siku kwa mtazamo wangu
 
Kuna mambo mawili unaweza kuyafanya. Nimeona njia mbili ambazo zote nina ushahidi nazo. Moja ni njia ya kutumia majani ya mlonge. Kuna mti unaitwa mlonge (ambao mbegu zake watu wengine wanazitumia kwa tiba mbalimbali). Mama yangu alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo akashauriwa atumie mlonge kama mboga. Akaanza kuchanganya majani ya mlonge kwenye mlenda, mchicha nk. Mboga yoyote ya majani aliipika pamoja na majani ya mlonge. Akala na sasa ni hadithi. Ninakumbuka mama yangu alikumbana na shida hii kwa miaka zaidi ya 30. Nikiwa mdogo alikuwa hali maharage wala machungwa. Ama la akila inabidi ameze dawa zinazoitwa magneziumu. (Mimi nilikuwa mdokozi nikiiba dawa hizo na kubugia kwa kuwa ni tamu kama pipi... )

Njia ya pili ni ya kiimani. Ni ya kiimani kwa maana kuwa, kuna magonjwa watu wa Mungu wanatupiwa na ibilisi. Nimeyashuhusia haya kupitia tv emmanuel ambapo watu wanafunguliwa na kutolewa kwenye vifungo vyao. Si lazima uende huko lilipo kanisa hilo ili ufunguliwe, ni imani yako tu ndiyo inaweza kuhamisha milima. Kuna watu wanafuatilia maombi kupitia televisheni zao na wanafunguliwa. Nimekuwa nikifuatilia tv emmanuel kupitia intaneti. 'Hakuna ugonjwa ambao Bwana Yesu alishindwa kuuponya..."
Nakutakia uponywaji mwema.
 
Wana JF Salaam.
Leo nakuja nikihitaji kupata ushauri wenu wa kitabibu.
Kwa sasa nina matatizo ya kiafya yanayonisumbua;
Kwanza kabisa kabla ya yote naomba nitoe background yangu ili iwe rahisi kupata picha ya matatizo yangu. Nina tatizo la vidonda vya tumbo, nilikuwa nakunywa bia kwa wingi na sasa nina karibia mwaka tangu nimeacha kabisa kunywa, napenda sana maharage, nakula pilipili sana, kwa ujumla sichagui chakula.
Sasa tatizo kubwa ambalo naona linazidi kushika kasi hivi sasa, tumbo langu linakuwa linaunguruma na kujikuta nikijamba sana karibia kila baada ya dakika chache japo mishuzi mingine haitoi halufu.
Lakini jambo lingine nimejikuta nikiwa siwezi kula aina yoyote ile ya matunda, na pindi ninapojaribu kula hutapika papo hapo, aidha hata nikiangalia tu mtu akiwa anakula najisikia kichefuchefu!
Hata upatikanaji wa choo si mzuri kwa sasa.
Je, tatizo ni nini na nifanyeje? Ikibidi ni PM jamani.
Mods naomba japo liwepo front kwa muda ili nipate ushauri.
bibie.@ Rahajipe Pole sana una Vidonda vya Tumbo na una matatizo ya ukosefu wa kupata choo kiurahisi hayo ndio matatizo yako makubwa ingawa hujatuambia umeshakwenda Hospitali kuwaona Ma-Daktari? Miminitajaribu kuweza kukusaidia hivi:

UKOSEFU WA CHOO: Soma tiba rahisi


UKOSEFU wa choo ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?

Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu

yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili

kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na

kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.

Maradhi ya VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS)

Ni kushindwa kwa kuta za tumbo kuvumilia makali ya aside ndani ya tumbo na kutengeneza vidonda vya tumbo.


Kuna makundi matatu ya vidonda vya tumbo
1.Peptic Ulcers
2.Deudenom ulcers
3.Gastric Ulcers


Kila vidonda vina aina ya maumivu yake
1.Tumbo kuuma juu ya kitovu
2.Kuuma mgongo
3.Kupata Kiungulia (heart burn)
4.Kukosa choo muda mrefu
5.Njaa kama umechelewa kula
6.Maumivu hupungua kama umekula
7.Huchagua vyakula
8.Huwa na dalili za kunenepa
9.Huwa hana njaa
10.Anaogopa kula
11.Hupata maumivu ya mgongo
12.Chakula akila baada ya nusu saa tumbo huanza kuuma
13.Tumbo huwaka moto
14.Ana dalili za kukonda


VISABABISHI vya vidonda vya tumbo:

Uvutaji wa sigara
Kutokula kwa wakati
Kutumia vyakula vya kusisimua mwili kama vile soda
Kula vyakula vyenye aside nyingi
Kushindwa kuthibiti hasira kama vile Hasira,huzuni na mawazo
Kutumia vyakula vikavu ambavyo huenda kukwangua tumbo
Kukaa mda mrefu bila kula
Kutumia vidonge visivyoyeyuka mapema



TIBA YAKE:

1.Maziwa ya soya

2.Vitunguu maji tafuna nusu yake kwa siku

3.Jitahidi kula kwa wakati

4.Usile ovyo ovyo

5.Pendelea kutumia matunda kama vile chenza

6 Kunywa Maji Uvuguvugu Unapo Amka Asubuhi kabla ya kupiga mswaki Unywe Glasi 2 za Maji ya Uvuguvugu na baada ya kupiga Mswaki

Unywe glasi 1 na kabla ya kunywa chai unywe Glasi moja ya maji ya Uvuguvugu kila siku Ufanye hivyo kwa wakati wa asubuhi.
Na Wakati wa

Mchana Dakika 15 au dakika 30 kabla ya kula chakula cha Mchana unywe maji ya Uvuguvugu Glasi 1.


Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.


na unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku. Jumla utakuwa umekunywa glasi 8 kwa siku huu ndio


utaritibu wa kutibu kila maradhi hapo juu uwe unakunywa kila siku mpaka upone hayo maradhi yako na huenda


ikachukuwa muda wa miezi 3 ukifulululiza kunywa hayo maji ya Uvuguvugu utakuwa umekwisha pona maradhi yako Vidonda vya tumbo.


Habari yako Mkuu PakaJimmy?
 
Back
Top Bottom