Rahajipe
Senior Member
- Oct 29, 2012
- 165
- 63
Wana JF Salaam.
Leo nakuja nikihitaji kupata ushauri wenu wa kitabibu.
Kwa sasa nina matatizo ya kiafya yanayonisumbua;
Kwanza kabisa kabla ya yote naomba nitoe background yangu ili iwe rahisi kupata picha ya matatizo yangu. Nina tatizo la vidonda vya tumbo, nilikuwa nakunywa bia kwa wingi na sasa nina karibia mwaka tangu nimeacha kabisa kunywa, napenda sana maharage, nakula pilipili sana, kwa ujumla sichagui chakula.
Sasa tatizo kubwa ambalo naona linazidi kushika kasi hivi sasa, tumbo langu linakuwa linaunguruma na kujikuta nikijamba sana karibia kila baada ya dakika chache japo mishuzi mingine haitoi halufu.
Lakini jambo lingine nimejikuta nikiwa siwezi kula aina yoyote ile ya matunda, na pindi ninapojaribu kula hutapika papo hapo, aidha hata nikiangalia tu mtu akiwa anakula najisikia kichefuchefu!
Hata upatikanaji wa choo si mzuri kwa sasa.
Je, tatizo ni nini na nifanyeje? Ikibidi ni PM jamani.
Mods naomba japo liwepo front kwa muda ili nipate ushauri.