Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa-Chunya Azungumzia Bajeti Wizara ya Kilimo

Masache Kasaka, Mbunge wa Lupa-Chunya Azungumzia Bajeti Wizara ya Kilimo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MBUNGE MASACHE KASAKA AZUNGUMZIA BAJETI YA WIZARA YA KILIMO

"Serikali umeweka utaratibu mzuri wa kuchukua vijana na kuwaweka katika makambi, nashauri tuwachukue vinana ambao wameshajiajiri tayari katika kilimo na tuweze kuwapa kipaumbele, hata benki inamkopesha mtu ambaye ameshaanza biashara" Masache Kasaka, mbunge wa Lupa-Chunya

"Sisi wilaya ya Chunya ni wanufaika wakubwa wa BBT (mradi wa mashamba makubwa kuwezesha vijana kulima kibiashara) kwa sababu tuna eneo lenye ukubwa wa hekta 47, 000 ambalo limeshatengwa kwa ajili ya mradi huu, ni mradi mzuri tunaipongeza serikali, mradi huu ukitekelezwa vizuri utakuwa ni ukombozi kwa nchi yetu na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha chakula kwa Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika" Masache Kasaka, mbunge wa jimbo la Lupa

"Naiomba serikali ione namna ya kuweka ruzuku katika mbolea kwenye zao la Tumbaku ili wakulima wa zao la Tumbaku waweze kunufaika kama walivyonufaika wakulima wa mazao mengine" Masache Kasaka, mbunge wa jimbo la Lupa wilayani Chunya

"Zao la Tumbaku lilikuwa ni kilio kwa wakulima hivi sasa limekuwa ni neema kwa wakulima, masoko ya zao la Tumbaku yanaendelea kufunguliwa. Nashauri makampuni ya kuchakata na kununua Tumbaku yaliyopo yalindwe na mengine zaidi yaje ili kuimarisha ushindani,kwa kuwa wakiwa wanashindana ndugu bei zinavyokuwa nzuri kwa wakulima " Masache Kasaka, mbunge wa jimbo la Lupa-Chunya

"Mbolea ya ruzuku imekuja kwenye package ya kilo 50 wakati huo huo wakulima wetu wana hali na uwezo tofauti kiuchumi, tuiombe serikali iwaelekeze mawakala wa mbolea kuweka katika vifungashio vya uzito tofauti" Masache Kasaka, mbunge wa Lupa-Chunya

"Licha ya mbolea kuwekewa ruzuku lakini kuna changamoto ya kufika kwa wakati kwa wakulima kwenye msimu uliopita, mbolea ya kupandia ilifika mwezi Desemba na Januari. Nitoe wito kwa serikali kuhakikisha mbolea ya ruzuku inawafikia wakulima kwa wakati"Masache Kasaka, mbunge wa Lupa

"Tunaishukuru serikali kwa kuweka ruzuku katika mbolea na kupelekea uzalishaji kwa wakulima wadogo kuongezeka na uhakika wa chakula kwa wananchi kuwa vizuri " Masache Kasaka, mbunge wa jimbo la Lupa wilayani Chunya

"Ustawi wa chakula katika nchi yetu inategemea wakulima wadogo ambao ni takriban asilimia 70 ya Watanzania wote, hivyo tuweke jicho la kipekee kwa wakulima hawa wadogo" Masache Kasaka, mbunge wa jimbo la Lupa wilayani Chunya
 

Attachments

  • Fvs0hsiWABMKAti.jpg
    Fvs0hsiWABMKAti.jpg
    76.1 KB · Views: 6
  • FvsmHjUaAAItnQZ.jpg
    FvsmHjUaAAItnQZ.jpg
    75.8 KB · Views: 6
Back
Top Bottom