Masahihiso katika Kiswanglish

hukumundo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2011
Posts
850
Reaction score
438
Ndugu,
Leo nataka ninyooshe lugha yetu tukufu ya Kiswanglish. Sababu ya kufanya hivyo ni kwamba, makosa yaliyo katika Kiswanglish ndiyo hayo yanahamishiwa kwenye Kiingereza, tunapojaribu kusema lugha hiyo. Tukizungumza na watu wanaojua Kiingereza, basi hapo inakuwa tatizo kidogo tunapoonekana tunababaisa. Nina maneno matatu ya kurekebisha leo:
1. Si sahihi kusema POSTPOND. Neno sahihi ni POSTPONE. Hiyo herufi ya mwisho haitamkwi. Utawasikia watu wanasema 'postponded.' Ni Kiswanglish kibaya. Past tense sahihi ni 'postponed.'
2. Si sahihi kusema 'ADVANCE level'. Sahihi ni ADVANCED level. 'Advanced' ndiyo hasa hutumika kama kivumishi. 'Advance' hutumika kama kitenzi au kama nomino.
3. Si sahihi kusema 'PROFESSIONAL yangu.' Sahihi ni 'PROFESSION yangu.' 'professional' ni kivumishi kama katika 'professional training.' 'Professional' hutumika kama nomino pale mtu anaposema 'I am a professional' kwa maana ya 'professional player' kwa mfano.
Nitajaribu kumwoma Mzee Kifimbocheza awaeleweshe vijana wetu wa shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…