Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 140
- 577
Wamasai hawana ardhi yao, ardhi ni yetu sotekwa Sheria ya ardhi ya 1999.
Aidha Rais Dkt. Samia aliwahamisha FAIRLY Ngorongoro hadi Tanga na kuwapa upendeleo kuliko kabila lolote; makazi, elimu, afya, malisho bure.
Wanaowafunda Wamasai migogoro dawa yao inachemka.
Tuelimishane...
Kwanza ieleweke Wamasai hawana ardhi yao, na sio wao tu, bali hakuna kabila lolote nchini lenye ardhi yao, kwani ardhi yote ni ya umma na Rais kwa niaba na manufaa ya umma anaweza kuibadili matumizi muda wowote kwa mujibu wa Sheria ya ardhi ya mwaka 1999.
Kuhusu takwa la kuhamishwa wamasai Ngorongoro halijaanza kwa Rais Samia kama Wapinzani na wanaharakati wanavyohangaika kutupotosha, bali ni takwa la Umoja wa mataifa chini ya UNESCO kwa Serikali za Tanzania kwa awamu tofauti katika kuilinda Ngorongoro kama Urithi wa Dunia iliyoanzishwa kisheria mwaka 1959.
Pia soma: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
Kwa mujibu wa Sheria hii, eneo hili linapaswa kukaliwa na watu wasiozidi 25,000 na malisho ya mifugo na wanyamapori isizidi 254,000.
Lakini takwimu za sasa kutosha mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro, wakazi jamii ya wamasai walishafikia 100,000. Ikiwa ni ongezeko kubwa kulingana na mahitaji ya binadamu, mifugo na wanyamapori.
Wale wanaobwabwaja mtandaoni kwamba si Rais Samia wala Serikali ya Chama cha Mapinduzi, CCM inayowajali Wamasai watafakari kwanza muda Serikali iliyotenga KUWAELIMISHA Wamasai bila kuwalazimisha kuhama. Serikali imetumia zaidi ya miezi 4 kuongea na viongozi wa kimila wa kimasai na Wamasai kuhusu maantiki ya kuhama, Serikali ya kidikteta ingefanya hili?
Lakini pia Rais Samia ambaye hawajali raia wake Wamasai angewezaje kuwajengea: Shule ya msingi yenye vyumba 7, shule ya Sekondari yenye vyumba 8 na Zahanati itakayowatibu katika kijiji cha Msomera Tanga⁉️ Bila kusahau maji ya kutosha kwa matumizi ya binadamu na mifugo yao⁉️
Lakini pia Rais Samia ambaye hawajali hawa Wamasai angewezaje kutenga eneo ambalo linamuwezesha mkazi Masai kufanya shughuli zake zingine hata kuweka boma la kufuga mifugo na eneo la malisho ambalo wataendesha shughuli zao za ufugaji?
Rais asiyewapenda Wamasai angejali kutangaza kupeleka malori kwa ajili ya kubeba samani na malori ya kubeba mifugo na kuwalipa fidia ya nyumba zao?
Tunaelewa kinachoendelea ni MRADI MKAKATI wa baadhi ya Wanaharakati, Wapinzani na ASASI za kiraia zenye LENGO KUU la kumchafua Rais Dkt Samia na Serikali yake ya CCM ndani na mbele ya uso wa kimataifa na hii ni baada ya mafanikio makubwa ya kila sekta yaliyoletwa na Rais Samia ndani ya miaka mitatu yaliyopelekea Rais Samia kupewa tuzo mbalimbali kimataifa, kuendelea kutufungulia dunia na kupendwa zaidi kila kona duniani. HAWAKUTEGEMEA!!
Kikundi hicho kinaumia sana kuona Nchi yetu, Rais wetu, Serikali yetu haisemwi vibaya kimataifa, furaha yao, na Maisha yao kutegemea madhaifu ya Rais na Serikali; awamu hii wameyakosa ndio maana sasa wanahaha KUWASHAWISHI Wamasai wagome na hata kuwaandikia mabango ya chuki dhidi ya Rais Dkt Samia.
Kikundi hiki kimeenda huko Ngorongoro na kimetumia advantage ya jamii ya wamasai kutoelimika, hivyo kuwarubuni kwamba wanaonewa kuhamishwa na Serikali, hivyo wagome, na kusababisha vurugu eti dunia ione. Huu ni uhaini kama uhaini mwingine.
Tungekuwa na Wapinzani na wanaharakati wazalendo wa Nchi yetu, toka awali wakati Serikali ya Rais Samia inawapa elimu, kwa kuzingatia unyeti wa Hifadhi Ngorongoro duniani, wangeenda kuwaelimisha pia, ila walikaa kimya, walipoona Wamasai wamekubali kuhama, wakaenda kuwashawishi wagome. WADHIBITIWE.
Mwisho nawaasa hawa Wapinzani na wanaharakati uchwara waache tabia hizi za uhaini, wamepewa Uhuru tele na Rais Dkt Samia, wamgawie wema, wasilazimishe kukamatwa na kufungwa kwa mujibu wa Sheria kwa kuhamasisha uvunjifu wa amani ya Nchi na uhaini, waje kuanza kulalamika.
Rais Samia ndiye Rais wetu sasa, mwakani 2025 na hadi 2030. Na hii haitokei wala haitotokea kwasababu ya mabavu, bali kazi nzuri anazotufanyia watanzania.
Suphian Juma Nkuwi,
Agosti 18, 2024
+255717027973