Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwani Malima yupo juu ya sheria? Hata kama angekuwa nani alipaswa kutii amri ya askari. Haijalishi yeye nani. Swala la uheshimiwa ni baadae.
Atii sheria kwa kosa gani Acha kuwa mbugila wewe askari ana mipaka yake pia,yule ni chizi askari huwezi pigapiga kelele hovyo
 
Huyo polisi anastahili kusimamishwa kazi.

Ndo mambo gani sasa hayo ya kufyatua risasi hewani kama siyo kutishia watu?

Ingekuwa ni juu yangu ningemfukuzia mbali kabisa maana hafai huyo....he is too trigger happy!


Hebu Sema hapo USA unapopatetea kila siku hali ilivyo, hali ya tukio lile lina mitazamo mingi ila hitimisho ni kuwa polisi kuwa salama na anayetaka kupigwa na wananchi alifanya vyema.

Bado, huyo jamaa amekamatwa kupelekwa kituoni kiusalama hujui wananchi wangekuwa na tafakari gani juu ya kukamatwa kwake.

Tena, jihoji kama aliyepaki gari hajakosea!?

Ila kwa kifupi, Askari ametumia busara sana ila mtu akiangalia hali hiyo kwa chuki zake kwa polisi basi ni lazima atamlaumu tu.

Zaidi ya yote, watanzania wengi ni wanafiki sana, mifano ni mingi !!
 
Kitendo cha polisi mwenye uniform kusema wananchi tawanyikeni inatosha sababu kila mwananchi anajua huyu ni police. Tena walikuwa wengi kwenye gari yao lakini walishuka wawili tu wakijua amri yao itafuatwa.

Kitendo cha kukoki bunduki na kupiga kinadhidirisha uwezo wa akili ya yule askari alikosea na uzuri citizen journalism imemchukua na video imerushwa mtandaoni
 
Kama kuna jambo baya duniani kwa kiumbe chochote kile chenye uhai, basi ni dharau.
Nimejaribu kufuatilia issue ya Malima kwa ukaribu...
Ukweli ni kwamba, kuna chembe chembe za kupimana ribs na kuoneshana dharau kati ya raia, waziri, mwanae na waziri dhidi ya Polisi...
Hata kama wewe una haki, kuna namna ya kuzungumza, the issue was already viral.... kumbuka issue ya kumuita "Mwizi alie kwenye gari"
Then Malima anaingilia katikati ya maongezi kati ya polisi na mtuhumiwa (Mwanae)

Mwananchi anadakia polisi akijibizana na Malima "Huna mamlaka wewe, huna mamlaka huyu waziri huyu, ana ulinzi"
Then Polisi anafyatua risasi hewani, Malima anasema " Kiongozi wa msafara wenu yuko wapi " aje hapa....

Hivi wananchi wanadhani hilo walilobeba polisi ni toy au?

Perception ya Dharau inaaniza kwa kijana, kisha baba anaingilia' yet, polisi anaonekana kama third class tu wakati wa mazungumzo, na wananchi wanashadadia....

Nakumbuka kimbembe cha waziri aliewahi ingia kwenye ATM posta bila kupita kwenye foleni....

Viongozi wetu tunawapenda, sheria mmetunga wenyewe, zikiwarudia mnaona mnaonewa... this is hugely unacceptable.....

Yani kwa dharau za kijinga namna ile ningekuwa mimi nisingevumilia hata kidogo.


Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.... The policeman was provoked to the first degree....
Ndio maana nimesema nimemkubali sana yule polisi aliyefyatua hakika ana uchungu na watu wenye dharau dadadeki.Kijana kunywa bili niletee sitaki ujinga mimi
 
Raia wanapoomba kumiliki silaha moja ya mambo wanayochunguzwa ni pamoja na ustahimilivu!Polisi hapaswi kuwa provoked kiasi cha kufyatua risasi hewani!Anapaswa apimwe akili
Ni rahisi kuchukulia vyovyote uwezavyo lakini kumbuka sio kesi ya kuua mtu basi mtuhumiwa atashtakiwa kwa kesi ya "murder" kesi zingine unaua na unashtakiwa kwa kosa la "man slaughter' kulingana na mazingira ya tukio.

Sio kila kesi ni murder na sio kila kosa ni kosa la polisi, ukitazama chanzo utagundua polisi alidharaulika kwa kua yeye ni polisi (kazi isiyokua na hadhi), hizi dharau viongozi wetu wa kisiasa wanazo sana, kama utakumbuka kesi ya Ditopile utagundua dharau ya viongozi wa kisiasa dhidi ya askari na dhidi ya raia
 
Kweli huwa wanakurupuka na kutunisha vifua kisa magwanda waliyovaa.
Ukikutana nao wengi wao hawana kauli za kistaarabu zaidi huwa wanadhania kila mtu ni kibaka!!
Ulimskia jamaa anasema "nimeapa Mimi huu mkanda una bendera, nimeapa" hivi alikuwa ana maanisha nini hasa!?

I personally don't find the logic out of that furious utterances
 
Even if the policeman was provoked to three first class degrees, alipaswa kucontrol temper yake. I guess at some point huko CCP Moshi wanafundishwa hivyo. Adam Malima was so calm and the poor policeman just embarassed himself
 
Sikujua polisi wote ni wana CCM, Ina maana upinzani ukishika madaraka polisi wote wataachishwa kazi?

Haya tungoje Red Brigades watakapo kuwa polisi

Kama hujui ndiyo ujue Polisi ni tawi la CCM.
 
Pamoja na hayo yote hakukua na sababu ya kupiga risasi hewani kabisa kabisa
 
ulimsikia askari aliyefyatua risasi akiongea kwa uchungu "kwanini hamuheshimu serikali??"
Tanzania viongozi wanajiweka matiti mbele na usiye kiongozi unanyanyaswa.
Wote tuwe watii wa sheria......tusiwaangalie polisi kwa makengeza kwakuwa kila mara wako wrong
Nimemkubali sana yule polisi natamani Magu amupandishe cheo ili watu waache ujinga wa kulewa madaraka.pumbafu
 
Ni rahisi kuchukulia vyovyote uwezavyo lakini kumbuka sio kesi ya kuua mtu basi mtuhumiwa atashtakiwa kwa kesi ya "murder" kesi zingine unaua na unashtakiwa kwa kosa la "man slaughter' kulingana na mazingira ya tukio.

Sio kila kesi ni murder na sio kila kosa ni kosa la polisi, ukitazama chanzo utagundua polisi alidharaulika kwa kua yeye ni polisi (kazi isiyokua na hadhi), hizi dharau viongozi wetu wa kisiasa wanazo sana, kama utakumbuka kesi ya Ditopile utagundua dharau ya viongozi wa kisiasa dhidi ya askari na dhidi ya raia
Wameshaona muongozo,aliyemtolea Nape silaha kapeta!Wamesoma game,huyu akipeta basi tutegemee matukio mengi tu ya askari kutumia silaha zao hata pale pasipotakiwa kufanya hivyo!

Swali la msingi;Ni wakati gani au mazingira gani askari anapaswa kupiga risasi hewani???
 
Asante sana Kanye2016 uliyechukua hii video...leo ndio nimejua polisi wetu wanafanyaje kazi hadi watu kama Ben Saanane wanapotezwa hivi hivi na maisha yanaendelea!

Laiti hii ingetokea nchi zilizostaarabika na ambapo utawala unaheshimu sheria, hii video ingekuwa tukio la mwaka na hata Waziri Mhusika ingebidi atoe maelezo.

Tazama huyo polisi mwingine anavyojitahidi kuokota maganda ya risasi kupoteza ushahidi... kama hii picha (video) haingekuwepo labda huyo Adam Malima ndiye angedaiwa kufyatua risasi.

Bahati mbaya nchi yenyewe ni Tanzania na michango ya baadhi ya watu humu wakitetea kitendo cha aibu kama hiki, ni uthibitisho tosha wa tuliko...kwenye handaki la ujinga; laws of the jungle!
 
Back
Top Bottom