Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Huyu mh alikuwa amesahalika sana ameamua kutafuta kick kwa nguvu ili akumbukwe.

Unajua tangu aibiwe guest house kule Moro alipotea sana. Sijui ile silaha yake aliipata?

Haya tumekukumbuka mh Adam km
 
Makelele yote hayo anamkamata mtu mwehe heshima zake kama Malima, angekuwa anamkamata kibaka au teja siangetamba kama dume la ng'ombe? Afyatua risasi hovyo tena masaki, angekuwa manzese je? Huu wote ni ujinga tu.

Na hili jambo la kijinga linapaswa kukemewa na kila mtu mwenye akili timamu. Hivi kazi ya usalama barabarani si ni kazi ya trafik hawa madalali wanahusikaje? Hii biashara ya kipumbavu ya kukamata magari barabarani ilitokea wapi?

Kama trafik wameshindwa kazi yao basi sumatra wachukue hili jukumu badala ya kutumia wahuni.
 
Nimependa sana jinsi Malima alivyojihamini,hakutikisika wala kutishika na SMG...Ni Kama Nape kipindi kile,inaonekana watanzania wameshapunguza uwoga wa silaha...Hii ni hatua nzuri.
 
polisi huyo alifuzu mafunzo kwel...anajua sheria na matumizi ya bunduki kwel cjui km hayo yalikuw mazngira maalum yakufyatua risasi
 
Akome ...mnashangaa ni kupigwa risasi juu!!

Kila Mtu anatumia nyenzo zake kujilinda..

mfano:walimu wengi huwaponda wanafunzi na chaki wanakosea darasani.
 
Hili jambo lina impact kubwa kiuchumi, huwezi kuungurumisha marisasi mchana maeneo ya masaki wanakoishi wawekezaji wataona tanzania sio salama kuwekeza.
 
Hii 'drama' ya ajabu sana.. Askari kitu cha kwanza kufundishwa ni nidhamu.. Ati Askari tena Mkuu wa msafara anapata hasira.. Anapoteza mwelekeo.. Anatulizwa na 'Junior' wake.. Hata maganda ya risasi anasahau kukusanya..
Hivi hawa Polisi wamefundishwa 101 za kazi kweli?
Unatumia bunduki kizembe (kwa mkono mmoja),unapoteza risasi('burst'),unashindana na raia..
Maisha ya askari yanategemea anavyoweza kupunguza matumizi ya ovyo ya risasi.. Risasi ndiyo ulinzi wake..
Huyu Afisa wa Polisi alipaswa kumweka huyu raia chini ya ulinzi siyo kuonyesha ubabe..
Hatuwezi kuvumilia kuwa na Polisi ambao ni 'cowboys' na 'trigger happy'..
 
Aniokoe yeye Mungu? Acheni kutukuza upuuzi, kwa miiko ya polisi hapo kesho anatakiwa site kupiga kazi ngumu. Madaktari nao wasemeje ambao unafika kwao hata hujatambui

Kila taaluma na kazi inaumuhimu wake.
Huyo Mungu mwenyewe aliweka jeshi kupigana vita na maadui wa Taifa la Israel Soma vitabu vitakatifu na misaafu utaona kuwa hata huyo Mungu anajua kulinda kwa kutumia askari na jeshi.

Kwa hiyo, heshimu polisi kwa sababu wanalinda maisha yako. Aidha, moja Kwa moja au vinginevyo.
 

wanahasira zisizosaidia

kama ningekuwa mtoa maamuzi yule asikari leo angelala rumande
 

Kama unamiliki gari basi jaribu kutembelea msasani na masaki yake uje usimame japo dakika mbili tu za kununua soda au maji kando ya barabara hata kama ni mita kumi kutoka ilipo barabara kuu halafu wale mbwa wanaoibia watu mchana kweupe wakukute ndio utuonyeshe mfano wa kuongea nao kauli nzuri.

Bila ya elfu 50 hawakuachi hata kama maneno yako yatakuwa na vina na virari.
 
Mungo park, kwanza alishaishiwa risasi akaanza kupanik na kuchimba mkwara apate msaada wa wenzie, halafu alipaswa aokote maganda hakufanya hivyo, tutajuaje labda risasi zingine alishauza.
 
Nimeangalia clip,Askari Polisi wa namna hawatakiwi kufanya kazi za operations kama hizo,anaonekana anafaa sana kuwa ktk kikosi cha kufuatilia wahalifu au majambazi wanaotumia silaha hukooo field ata enjoy sana kazi yake ya Polisi.
 
Kuna haja ya kutazama umri wao hawa jamaa, iwe kuanzia miaka 28 na kuendelea,naona utoto umezidi sana sasa.
Mtu anajiita serikali huku anafanya utoto hivyo?Halafu kavaa bendera yetu huku anaitambia?Maneno yake yanaonyesha bado hajakomaa kichwani,maana anajisikia inferior kwa raia mwenye v8 kiasi cha kulazimisha aonekane wa maana wakati tayari yeye ni wa maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…