Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwanza nini maana ya dharau? Nyie wavuta bangi mlipata kazi Jeshini kwa vyeti feki dawa yenu inakuja. Kule CCP mlikuwa mnajifunza nini?

Aaah mkuu bangi inaingiaje hapo? Kuwa na heshima. Sio unaingiza na vitu ambavyo havipo.
 
wanaume wa dar, polisi akiwasogea tu wote wanakimbia ha ha ha ha ha........khaaaa.....
 
Huyu Askari ni wa kufukuza kazi mara moja,period
He is reckless and so unprofessional
 
Naona anatafuta cheo. Mi sijui nitumie mbinu gani Magu anisikie nipate hats ukatibu tarafa.
 
Hivi vi askari vimetoka mafunzoni juzi basi vinadhani vinaweza kumbabaisha kila mtu. Hivi ndivyo vya kupeleka kule Kibiti vikafundishwe kazi...
 
Hakuna hawa askari hua wanakurupuka sana wakishakua tu na hivo vibunduki wanajua watu watawaogopa.
Kweli huwa wanakurupuka na kutunisha vifua kisa magwanda waliyovaa.
Ukikutana nao wengi wao hawana kauli za kistaarabu zaidi huwa wanadhania kila mtu ni kibaka!!
 
Polisi alikuwa anatafuta nini pale? Na baada ya kujua kwamba eneo ni salama walifanya nini? Nataka kujua chanzo cha hili " zogo" ni nini?
mtoto wa waziri amepaki sehemu isiyoruhusiwa.. majembe auction (mwenye towing authority) amemuomba atoe gari mtoto wa Malima kakataa.. Majembe kaita polisi... mzee malima nae kaja.. polisi wanaamuru gari litolewe malima anamu ignore polisi.. polisi mmoja kapanda jazba "kwanini hamueshimu serikali?" na kupiga risasi juu... Thats all i know mkuu
 
Kiufupi inabidi hao Yono na Majembe wanaudhi sana inabidi tuanze watia adabu kwanzay
 
Hivi kuheshimu Serikali au kuigopa Serikali?? Kwanini mwenzake alimwambia aache?Alijua wanamakosa.Ifike mahali pande zote mbili ziheshiamiane.Polisi lazima waheshimu RAIA na RAIA waheshimu polisi bila polisi kuheshimu RAIA hakuna kujeshimiana.Angeua RAIA wange sema polisi kaua Jambazi Sugu.

Mbona enzi za JKN huu upumbavu ilikuwa hakuna.Ushenzi huu upo awamu hii tu kisa polisi aogopewe.
Acha uongo wewe! Ina maana umesahau enzi za "wapigwe tu maana hakuna namna, maana maana tumechoka sasa!" (per peter)
 
ulimsikia askari aliyefyatua risasi akiongea kwa uchungu "kwanini hamuheshimu serikali??"
Tanzania viongozi wanajiweka matiti mbele na usiye kiongozi unanyanyaswa.
Wote tuwe watii wa sheria......tusiwaangalie polisi kwa makengeza kwakuwa kila mara wako wrong

Na akamweleza kabisa yeye ameapa kuilinda jamhuri...Watu wasipoelewa na kuwa heshimu watu wenye dhamana huku wakitaka wao kuheshimiwa, then I am speechless...Kuna mazoea yalijengwa na kuna watu walishajiweka kwenye class fulani, sasa wanapotakiwa kurudi katika position zao wanashindwa...
 
Kweli huwa wanakurupuka na kutunisha vifua kisa magwanda waliyovaa.
Ukikutana nao wengi wao hawana kauli za kistaarabu zaidi huwa wanadhania kila mtu ni kibaka!!
I hate police, i feel the same way... ila siwapendi viongozi na ma ex-viongozi na familia zao kwa kujidhani wako above the law
 
Mie
Nimeshangazwa na huyo afande mbona povu limemtoka ivyo!!!
 




Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Adam Kighoma Malima akuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.

Sioni kutishiwa kokote hapo au clip nyingine??
 
mtoto wa waziri amepaki sehemu isiyoruhusiwa.. majembe auction (mwenye towing authority) amemuomba atoe gari mtoto wa Malima kakataa.. Majembe kaita polisi... mzee malima nae kaja.. polisi wanaamuru gari litolewe malima anamu ignore polisi.. polisi mmoja kapanda jazba "kwanini hamueshimu serikali?" na kupiga risasi juu... Thats all i know mkuu
Malima na mwanae wana makosa.sheria na utaratibu lazima ufuatwe.lakini pia sikuona sababu ya askari kupiga risasi
 
Back
Top Bottom