Masaki na Oysterbay : Wapangaji Wagonga Chupa! Kodi kulipwa kwa Dolari!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Wakazi wa Masaki na Oysterbay ambao ni wapangaji kwenye nyumba za mabwanyeye wamejikuta wakishangilia na kuamshana kwenye makundi yao ya WatsApp baada ya ddola kuporomoka dhidi ya shilingi.

Nyumba za Oyesterbay na Masaki nyingi zilikuwa ni za umma/serikali watu wakauziwa bei ya soda, wao wakamua kuzikarabati na kodi ya mwezi ni zaidi ya bei waliyouziwa.
Kodi ya Masaki na Oysrerbay inalipwa kwa dola japo Serikali ilishapiga marufuku.

USHAURI: Kwa mpangaji wa Masaki na Oysterbay, kama mkataba wako unakaribia kuisha, ongeza hata miaka mitano na lipa yote kwa dola, alafu tulia.
 
Watanzania wengi wasichoelewa ni kwamba hii trend ya dola kushuka thamani ni ya muda mfupi tu, muda si mrefu dola itarudi kupanda bei.

Kwa sababu bei ya dola inaenda na fundamentals za uchumi wa nchi za import / export na Tanzania haijaongeza exports za ku sustain shilingi kupanda bei kwa muda mrefu.

Kwenye soko la muda mfupi mpaka wa kati serikali inaweza kushusha bei ya dola hata kwa ku flood dola za mkopo kwenye soko, ila haiwezi ku sustain hiyo hali kwa zaidi ya miezi sita au mwaka.
 
Karibu naanza kuchoka kuchangia humu, maana unaweza ukajikuta kia waati unachangia jambo lilelile.
Ni kweli hii trend haina maana yoyote kwa sarafu na uchumi wa Tanzania, na isitoshe limekuwa ikitokea mara kwa mara ikitegemea na matukio.
Tukio la Uchaguzi wa Marekani pekee linaweza likabadili hali ya hewa duniani. Pamoja na hili kitokea kila wakati, inaonekana watu wana tatizo la kupoteza kumbukumbu, na wanaliona ni tukio jipya kuwahi kutokea duniani.
Ngoja tuone, maana hivi sasa linatumika kupata political gains wakati mambo yanazidi kuwa tete.
 
Wenzako huku tz kinachoendelea stori za kumshukuru mama kwa kwenda mbele...
Mie nakaaa kipembeni nikicheka
 
Usichoke mkuu.

Ujue uzi hata ukiwa na 99% comments za abracadabra halafu 1% tu ndiyo ziwe posts za maana, watu wanaojua mambo wataona tu, na hizo post 1% za maana ndiyo zitahitajika zaidi kuelimisha.
 
haya mambo ya shobo ya dola hapa nchini sijawahi kuyaelewa. na hata serikali nao ndio hivo hivo, kuna kodi wanalipisha kwa dola, NI upumbavu wa kiwango cha juu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…