Watu wamekazana na hoja kwamba "matajiri hamuwajui!" Matajiri wanatofautiana kulingana na kariba zao kwahiyo tuache ulimbukeni! Hapo wanaotajwa ni wasanii kwahiyo tutakuwa watu wa ajibu ikiwa tunawaona si lolote eti kwavile tu tunaamini matajiri ni akina Bakhresa! Hata huko US, ripoti zinasema Dr. Dre ndie mwanamuziki tajiri zaidi lakini kwa kutumia vigezo vyetu vya kutaka kuwaweka akina Masanja na akina Mengi basi hata huyo Dr. Dre ni fa'ra tu mbele ya matajiri! Hata huyo Bakhresa na yeye ni mbwiga tu mbele ya matajiri lakini kwavile reference yetu ni Tanzania, tunamuita tajiri ingawaje utajiri wa Dangote peke yake ni zaidi ya mara 20 ya ule wa Bakhresa!