Masanja awa mbele ya Jaydee na Profesa Jay kwa Utajiri Tanzania

Masanja awa mbele ya Jaydee na Profesa Jay kwa Utajiri Tanzania

Huyu sio tajiri sema anajiweza ina maana kuna baadhi ya wabongo hawajui maana ya mtu tajiri duh! basi tupo nyuma mno mleta mada inaonyesha huna shule pili unakaa uswahilini.
 
IMG_3609.JPG


UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wACanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

HABARI MEZANI
Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.

“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.

Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”

Chanzo: GPL

Maana ya utajiri ni nini?
Maandiko yanasema " Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu ka sindano kuliko TAJIRI kuurithi ufalme wa mbinguni".
Kama mwandishi anafikiri Masanja ni tajiri amekosea sana! Masanja ana uwezo wa kawaida tu katika kuyamudu maisha. Ni watanzania wengi tu wamefika au kuzidi kwenye hatua hiyo aliyofika Masanja lakini hatuwezi kusema kuwa wana utajiri wa kutisha. Mleta uzi tushawishi upya kwa kuanza na maana ya neno "utajiri "
Na pia mkumbushe Masanja kuwa kama ni tajiri basi pamoja na uchungaji wake ufalme wa mbinguni atausikia kwenye bomba.
 
Kama sehemu ya pesa anatengeneza kwa kivuli cha injili basi sio sawa kumshindabisha na wasanii...ashindanishwe na matapeli wenzake wanaotumia injili na maandiko kulaghai wanainchi wenye uvivu wa kufikiri.

Ajabu wale jamaa wa desi walishughulikiwa na serikali lakini hawa "watumishi" wanatumia njia hizohizo za "panda mbegu uvune" wanaachwa wanapeta tu.
 
Ivi wanaujua utajir hawa? Kila siku wanatangaza mali hizo hizo nfuuu

Mkuu these people are really simple minded kweli! Kutwa kucha kujadili mali za mtu, kubwa zaidi ku-amplify hata yasiyo-"ampliafika"
 
Watu wamekazana na hoja kwamba "matajiri hamuwajui!" Matajiri wanatofautiana kulingana na kariba zao kwahiyo tuache ulimbukeni! Hapo wanaotajwa ni wasanii kwahiyo tutakuwa watu wa ajibu ikiwa tunawaona si lolote eti kwavile tu tunaamini matajiri ni akina Bakhresa! Hata huko US, ripoti zinasema Dr. Dre ndie mwanamuziki tajiri zaidi lakini kwa kutumia vigezo vyetu vya kutaka kuwaweka akina Masanja na akina Mengi basi hata huyo Dr. Dre ni fa'ra tu mbele ya matajiri! Hata huyo Bakhresa na yeye ni mbwiga tu mbele ya matajiri lakini kwavile reference yetu ni Tanzania, tunamuita tajiri ingawaje utajiri wa Dangote peke yake ni zaidi ya mara 20 ya ule wa Bakhresa!
 
Back
Top Bottom