Masanja awa mbele ya Jaydee na Profesa Jay kwa Utajiri Tanzania

Masanja awa mbele ya Jaydee na Profesa Jay kwa Utajiri Tanzania

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
IMG_3609.JPG


UTAJIRI wa komediani maarufu Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji' ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wACanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

HABARI MEZANI
Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.

"Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja," kilipasha chanzo chetu.

Kikaongeza: "Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

"Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani."

Chanzo: GPL
 
ananiboa tu anapotumia jina la YESU KRISTO kujinufaisha jinsi isivyo sahihi.

Kwa mtazamo wangu akiwa kwenye kumtumikia MUNGU aache u-comedy
 
Masanja aendelee hivo hivo coz najua Mungu nae Ana sense of humor so Kama amkufuru kwa comedy bas najua na Mungu atakuwa anafurahi pia kwa jinsi Masanja anavyo tumia kipajo cha kulitukuza jina lake hail Masanja. Piga kazi bro n don't forget to make more money.
 
Inawezekana ni tajiri ila sina uhakika ni bilionea.
 
Hyo injili anaifanyia wapi? Ananiboa anavyojichetuaga kama tahira nfuuu

anaombeaga watu binamu....kuna moja niliona eti kamponya mtu
alikuwa mlevu... nilicheka sana.... wakati namjua alivyokuwa anatembea
na shoga angu H.. bidada ikabidi amuache kwa namna anavyogonganisha maduu
 
Umepitia financial statement zake za mwaka Jana nini?
Sababu umedadavua vzr hahaha
 
Laiti mgelijua kilichokuwepo nyuma ya pazia usingeandika hapa..huyu mtu huyu..ila time will tell..ukweli utajulikana tu..
 
Hivi Tanzania ni umasikini uliokithiri au ushamba maaana ukiwa na nyumba na gari kadhaaa, mashamba unakua tajiri daaah niji qualifications za huo utajiri
 
Kwakweli dini nyingi ni Usanii mtupu. Hivi mungu gani anaruhusu uvaaji na kusuka nywele kama afanyavyo Masanja???
 
Back
Top Bottom