Masanja Kadogosa katumbuliwa kama Katibu wa Bodi ya TRC. Je, anabaki na Ukurugenzi wake? Kama anabaki nao ni halali?

Masanja Kadogosa katumbuliwa kama Katibu wa Bodi ya TRC. Je, anabaki na Ukurugenzi wake? Kama anabaki nao ni halali?

Kwanza kabisa niwatakie Jumatatu ya Pasaka yenye Baraka.

Sasa naomba majibu ya swali langu.

Masanja Kadogosa ni Katibu wa Bodi ya TRC na anaingia Hapo siyo kwa kuteuliwa bali kutokana na Cheo chake cha Mkurugenzi mkuu wa TRC.

Sasa Masanja Mkandamizaji katumbuliwa kwenye Bodi je bado ana uhalali wa kuendelea kuwa MD na ikiteuliwa Bodi nyingine arudi tena kama Katibu?

Nipo hapa kuelimishwa

Shujaa: Nitawaletea Treni ile Watoto wa Mjini wanaiita "Mjusi"
Hata mimi logic sioni!!
 
k

kuna vitu huelewi
ama unavyo hisi viko hivyo ni hapana
ukiwa katibu wewe ndo mtaalamu na hushauri nini kifanyike, kama ulicho shauri wajumbe hawajakubaliana nacho kwenye muhtasari una andika ushauri wako ulikuwa vp na wajumbe waliamua vipi

kuwa mwenyekiti na kusaini document haikufanyi usaini unacho taka wewe tu. kuna wakati wajumbe wana amua usiyo yataka na document una saini mkuu

sasa kama ni kusaini upendayo wewe tu kuna haja gani kuwa na wajumbe si akae mwenyekiti na katibu wapitishe wanayo taka wao kisha wasaini

maamuzi ya bodi huenda kwa kupiga kura ama upande wenye kura nyingi ndo huamua jambo si mwenyekiti wala katibu
Kama mnataka Kadogosa awajibike au awajibishwe, kuweni wawazi. Sio kubisha vitu ambavyo viko wazi. Nashiriki vikao, najua nafasi ya mwenyekiti, najua influence ya mwenyekiti. Mwenyekiti mnyonge hafai kuwa mwenyekiti.
 
Acha kupotosha

Katibu wa Bodi ndio mratibu na muandaaji wa Mikutano yote ya bodi ikiwemo kuandaa board paper

Ushawishi wake ni mkubwa zaid ukiondoa wa mwenyekiti

Unacho kisema ni sahihi kabisa ataandaaje board paper kama as of is "deaf and mute" - wakati yeye ndiye mkurugenzi mkuu wa Shirika, kama angekuwa na uzalendo wa kweli kwanini anlikosa ujasiri wa kumu-confront board Chairman na kumwambia point blank kuwa huko tunako elekea siyo kabisa - lakini kunyamaza kwake na kujali zaidi kuandaa ma board papers ambayo yameshenini more questions than others in other words kunyamaza kwake speaks volume about him, siwa kichukuliwa lightly hata kidogo - who knows may be aliwahi kumutonya rais kuhusu mwenendo wa board nzima kwamba haufahi au aliwahi kutoa taarifa takukuru - kama alikaa kimya wakati mambo hayaendi vizuri basi na yeye ana walakini mkubwa kwenye suala hili - naye aondolewe kama wenzake hii lame excuse ya kusema eti "kazi yake ilikuwa ni ku present board papers tu hiyo ni immaterial.

Ukweli ni kwamba hakuna chochote kilicho kuwa kinafanyika cha ndio sivyo pale bila ya DG/CEO kujua, haiwezekani - mzianze ku-manufacture lame excuses eti "wanataka kuwaonea Wasukuma walio bakizwa kazini na Mugufuli", after all - Dr. SSH hayuko hivyo hata kidogo.
 
Kama mnataka Kadogosa awajibike au awajibishwe, kuweni wawazi. Sio kubisha vitu ambavyo viko wazi. Nashiriki vikao, najua nafasi ya mwenyekiti, najua influence ya mwenyekiti. Mwenyekiti mnyonge hafai kuwa mwenyekiti.
mkuu utakuwa unashiriki sawa ila hujui unashiriki nini

mwenyekiti ana ifluence sawa ila hana madaraka yote kama unavyo taka kutuaminisha

anacho fanya ni kushawishi wajumbe kukubaliana nae

ila kama wajumbe idadi kubwa wakikinzana mawazo na mwenyekiti hawezi amua ilo jambo kwa utashi wake (kama unavyo taka kutuaminisha)

mwenyekiti ni mjumbe kama wajumbe wengine sema yeye kapewa kuongoza tu

ntakuwa wa mwisho kukubaliana na wewe kuwa mwenyekiti ana nguvu ya kusaini dokumenti kwa utashi wake hata wajumbe wapinge wote.
 
Yes yeye anaendelea kwasababu yeye ni mtu safi, hahusiki ila najua kuna watu wana hamu sana Wasukuma wote walioteuliwa na Magufuli, watumbuliwe kwasababu wanadhani waliteuliwa kwa Usukuma wao na sio kwa sifa zao na vigezo.

Mama akifanya kosa hili, la kuwatumbua Wasukuma kwasababu tuu ni Wasukuma na waliteuliwa na Msukuma, atakuwa anatenda dhambi kubwa ya ubaguzi!. Japo Rais Magufuli ni Msukuma, sijui ni wangapi humu wanafahamu kwanini ni Magufuli, Mimi ni mmoja wa watu wachache sana wanafahamu why ni Magufuli Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Na japo Magufuli alijaza Wasukuma baadhi ya maeneo, niliwahi kulishauri Bunge letu lichunguze Wito kwa Bunge letu tukufu: Mkithibisha hii Nepotism ya ajabu na zile Boeing ni TT, then hatufai!.

Hivyo japo ni kweli Magufuli aliwateua Wasukuma wengi lakini hakuwateua kwa sababu ya Usukuma wao, aliwateua kwasababu ya kukidhi sifa na vigezo Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Hivyo Mama akifanya kosa la kuwatumbua Wasukuma kwa Usukuma wao, atakuwa amefanya kosa kubwa la dhambi ya ubaguzi, karma haitamuacha Mama salama!.

Japo hakuna mtu yoyote ajuaye ni kwanini JPM ameitwa mapema, lakini wapo watu wanaojua na sababu wanazijua, hivyo wana jukumu la kumsaidia Mama kuepuka mambo yanayotengeneza bad karma

Inabidi kwenye vile vikao kazi vyao na semina elekezi wawe wanaita na watu wa holistic advice ili wafundishwe kitu kinachoitwa karma, it's real na kuhakikisha wanapoboronga, wanapisha tuu wenyewe ili kumlinda Mama Wito Kwa Viongozi Wetu: Unapokosea, hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge utamaduni wa kuwajibika ili kumuepushia Rais wetu kubeba mzigo wa karma
P
Kadogosa hawezi kufanya manunuzi makubwa hivyo bila Makatibu wakuu wa wizara za uchukuzi na hazina, mawaziri wao na mwisho Ikulu lazima ijue, hapa wanaotakiwa kuondoka ni kuanzia Waziri Mkuu mpk huyo Kadogosa
 
Mwanzoni kipindi cha magufuli nilijua mkurugenzi ndugu kadogosa ni mtu makini na mzalendo kumbe ni uchafu kama walivyo akina nape
Tatizo la Tanzania ni system nzima imeoza kuanzia Ikulu kushuka chini hakuna msafi hata mmoja, wote ni wezi tupu
 
Back
Top Bottom