Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amewaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuhubiri mema ikiwamo kuimarisha muungano na umoja kama Taifa.
Kadogosa ameyasema hayo Aprili 21, 2025 jijini Mwanza alipokuwa mgeni rasmi katika ibada ya Pasaka na maombi maalumu ya kuliombea Taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria.
Akizungumza katika ibada hiyo amewaomba viongozi wa dini nchini kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ya kijamii kuhakikisha wanahubiri mahubiri mema yatakayoendeleza muunganiko uliopo na umoja kama Taifa.
"Kama Taifa, katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi tunahitaji umoja ili tuvuke kwa amani na utulivu. Hivyo, viongozi wetu wa dini msiache kutuombea," amesema Kadogosa.
Amefafanua kuwa umoja ndiyo utaliwezesha Taifa kushiriki uchaguzi wa mwaka huu na huku shughuli za maendeleo na nyinginezo zikiendelea kwa utulivu na amani.
Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria (DMZV), Stephen Ling’wa amesema kuwa amani, utulivu utaendelea kuwa ngao ya kumaliza Uchaguzi Mkuu kwa salama.
“Siku zote tutaendelea kuhimiza muunganiko, amani na utulivu nchini, tukihubiri amani kila mmoja ataona umuhimu wa hilo, kwani hata kusanyiko hili ni la kuliombea Taifa amani,”amesema Ling’wa.
Source:
Wasafi Fm