Wandugu, huyu aliyekuwa Mkurugenzi wa TRC ni kuwa alitumbuliwa kwa kuvurunda huko au anasubiria kupangiwa majukumu mengine makubwa....
Binafsi naweza kumpa maua yake kwa kusimamia uanzishwaji wa SGR hadi ilipofikia sasa....au alifikia umri wa kustaafu?
UUkitaka kujuwa ni kati ya hayo mawili anza na kudadisi 'timing'!
Kama ni "kusubiria kuangiwa majukumu mengine makubwa", iwe ni kwa muda mbovu kama huu; mbona atasubiria sana; na hata engine asahaulike kabisa!
Labda, kama majukumu hayo makubwa mengine ni katika jitihada za kuwanufaisha wateuzi wenyewe kwa kumtumia kama 'chambo'.
Binafsi sina ushahidi wa kumnyima "maua yake".
Kwa kushudia tunayo yaona tukiwa huku nje, ni heshima kubwa kuisimamia ile kazi ya ujenzi na hata uendeshaji wa SGR hadi hapo ilipofikia.
Kumbuka mfano wa wenzetu jirani zetu hao kaskazini. Kazi zote zilisimamiwa kwa sehemu kubwa na wachina, na hata iliowadia wakati wa kuendesha shughuli za uendeshaji wa huduma, hao hao wachina ililazimu wafanye kazi hiyo, ambayo ndiyo sasa wanaimalizia kabla ya kuwakabidhi wenyeji washike hatamu.
Nayasema haya kwa majivuno makubwa, kama ni kweli tumeweza sisi wenyewe kuendesha shughuli hadi haa kwa mafanikio. Siyo sifa nzuri kila mara kuwategemea akina DP World katika kila tunachoweza kufanya sisi wenyewe. Ni lazima tujenge tabia ya kujiamini, kuwa tunaweza kufanya mambo yetu wenyewe kwa ufanisi.
Nirudie tena, haya ni maoni ya mtu wa nje, ambaye hajasikia yanayotogota ndani kwa ndani; kama ndiyo sababu ya kuwekwa embeni.