SI KWELI Masanja Mkandamizaji amechapisha 'Wakatoliki wasipoteze muda kumtafuta padri Nikata'

SI KWELI Masanja Mkandamizaji amechapisha 'Wakatoliki wasipoteze muda kumtafuta padri Nikata'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Jamii Check Kuna Graphics Ambayo Inasambazwa Katika Mitandao Ya Kijamii Ikionesha Chapisho La Masanja Mkandamizaji Kuhusu Suala La Kutekwa Kwa Polepole Na Padre Nikata Kuwa Ameuawa .je Chapisho Hilo Ni La Kweli Ama Uongo.
MASANJA.jpg
 
Tunachokijua
Oktoba 10, 2025 Mhashamu Damian Dallu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea alitoa taarifa kuwa Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea, ambaye ni Mhadhili katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza, haonekani wala hapatikani kwenye simu yake.

Baada ya taarifa hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma lilieleza kuwa linaendelea na Upelelezi wa tukio la kupotea kwa Padre huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamisha Msaidizi Mwandanizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya alisema Padri Nikata alifika Songea tarehe 03.10.2025 akitokea Dodoma huku akiwa na mhadhili mwenzake ambaye ni Padre wa Jimbo la Songea na kufikia katika nyumba ya Mapadre, St. Shanney, Ilipofika tarehe 07.10.2025 majira ya jioni Father Nikata alionwa na padre mwenzake huko Mtaa wa Kanisani akiwa na kibegi kidogo Mkononi akielekea Stendi ya zamani ya Mabasi Mfaranyaki ambapo tokea tarehe hiyo hakuweza kurudi mahali alipofikia jimboni.

Madai

Kutokana na taarifa hiyo kumekuwepo na picha ya ujumbe unaodaiwa kuchapishwa na Masanja Mkandamizaji katika ukurasa wake kwenye mtandao wa X ukisema "Ndugu zangu Wakatoliki Padri Nikata alishatupwa baharini kama Pole pole tu msipoteze muda wenu kuwatafuta marehemu hii ndio maana halisi ya kazi na Utu"

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kupitia ukurasa rasmi wa Masanja kwenye mtandao wa X.

Aidha ujumbe huo una mapungufu yanayodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji. Picha yenye ujumbe huo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X, mfano kutumika kwa tiki ya bluu (blue checkmark) yenye umbo tofauti na inayotumiwa na mtandao huo.

Kukosekana kwa alama ya Grok, nukta tatu upande wa juu kulia, umbo la picha katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka mtandao wa X, muonekano wa picha ya wasifu isiyotumiwa na mhusika. Pia kukosewa kwa majina tofauti na majina halisi ya mhusika.
​
1760190631279-png.3487060
Back
Top Bottom