Kwanza hakumtaja Mengi.
Pili hata kama angemtaja Mengi, jamii yenye uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza isingejali, as long as angekuwa na vithibitisho.
Tatu, katika jamii inayojali uhuru wa kujieleza, hata mawazo ya kijinga yana ruhusa kupata nafasi.
Nne, hukulazimishwa kuangalia.Katika jamii yenye kufuata mfumo wa soko huria kuna vyombo vya habari vinavyotangaza ujinga makusudi kwa sababu pengine ujinga ndio unauza(The New York Post, Uwazi). Wewe kama unaona huu ni ujinga usinunue bidhaa, usinunue gazeti, usiangalie kipindi. Mwisho wa siku wadhamini watajua kipindi hakiangaliwi, wataondoa matangazo yao na hao mabosi wenyewe wataona ulazima wa kubadilisha.
Ndio maana kuna watu hawanunui vitu Wal-Mart (low price supermarket) kwa sababu wana protest hali mbaya za wafanyakazi.Badala yake wananunua vitu kwa bei ya juu zaidi lakini wanajua hawachangii katika kuitajirisha Wal-Mart.
Watu wali protest kununua ndizi za Costa Rica kwa sababu mabwanyenye walikuwa wanapuliza madawa kwa kutumia ndege na kupulizia sumu kwenye visima vya wafanyakazi wa mashamba ya ndizi waliokuwa wanaishi katika mashamba hayo (plantations).
Kwa hiyo kama hupendi kitu, anzisha "boycott" campaign. Ama sivyo utakuwa unaleta advertisement zitakazoongeza ratings zao tu.