Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Mimi niliangalia kipindi kile, ijapokuwa nilikuwa na hama hama kati ya TBC1 na EATV, pale mwishoni alipokuwa anafunga kipindi Masanja alitoa maneno yaliyokuwa yanaonyesha hasira yake juu ya EATV na R. Mengi.
Ingawa hakutaja jina, lakini sentensi kama hii ahihitaji mtu kujua sayansi ya kurusha roketi kujua alimaanisha nini, alisema...."watu wana hela lakini wana roho mbaya (huku akionesha ishara ya kukunja kidole) wana hela nyingi lakini hawatosheki......na je kwa nini wameweka muda huu huu......si wangetafuta muda mwingine?" Alafu akaendelea..."najua sasa hivi watazamaji mnaenda kwa jirani ku angalia....lakini sisi ndo wenye vipaji vya ukweli...hatuna hela lakini tuna vipaji...."
Ni wazi alikuwa akiwasema EATV na kipindi chao kipya cha Ze Comedy....ambacho kinarushwa muda sawa sawa na kipindi cha Orijino Komedi cha kina Masanja!!!
Masanja anasahau kwamba EATV walikuwa wanarusha hicho kipindi muda huo huo hapo mwanzo....na ni TBC1 na kina Masanja unaweza ukasema ndo waliiga muda (ambapo kwangu naona sio issue).
Nakumbuka hata kipindi kile Futuhi wa Star TV na Vimbwanga time wa Channel 10 wanaanza, kina Masanja waliwapiga madongo sanaaaa!!
Ninachokiona hapa ni kwamba kina Masanja, Joti na Seki hawajui maana ya soko huria ambapo kila mtu ana uhuru wa kuingina sokoni na kuuza bidhaa au huduma anayoitaka. Katika mfumo huu ni soko tu ndilo litakalomfanya mtu aitoe bidhaa yake sokoni, kwa mfano Vimbwanga time cha Channel 10 walivyoacha kurusha kipindi hicho.
Masanja et al acheni kutukana watu........TV station zenyewe ziko 3 tu hapa nchini sijui mtakimbilia wapi mkitemwa TBC1. Kila mtu atakayetaka kufanya kazi na nyie ataogopa kudhalilishwa siku mtakapo vunja mkataba!!
Naona upeo wenu wa kufikiria ni mdogo sana, nawashauri acheni majungu na visilani.......pigeni kazi, kipindi bora ndicho kitakachoangaliwa na watamaji na si vinginevyo!!
Ni hayo tu!
Kiongozi umeona senksi niliyokukabidhi kwa hii yuzifuli posti?
You have said it. You have said it well.
Nadhani mjadala umeuhitimisha vizuri.
Kwamba The Orijino komedy Hawana adabu, waoga na hawana shukrani: Period!