Masanja na Uropokaji kwa Wazee!


Kiongozi umeona senksi niliyokukabidhi kwa hii yuzifuli posti?
You have said it. You have said it well.
Nadhani mjadala umeuhitimisha vizuri.
Kwamba The Orijino komedy Hawana adabu, waoga na hawana shukrani: Period!
 
Kijana nna mashaka na wewe. Unaanza na posti ya kwanza kwa pumba?Kuwa muungwana bisha hodi kwanza ukaribishwe!

Nenda kwenye jukwaa la utambulisho kwanza ujitambulishe huko, ndo uanze kuflow
Ahaa! Kumbe na wewe kiongozi umemtukia? Anaitwa Bandaz! Kule kwetu ukisema Bandaz........! Hehehehe!
 
Wenye shida siyo kina Masanja bana,hao ni nyasi tu kwenye bonde la mpunga mwenye maamuzi ni mkulima kupalilia nyasi na kuacha mpunga au kupalilia mpunga na kuacha nyasi. Hivyo basi hata mwajiri wao pia ana matatizo makubwa katika jamii.Kama Utawala wa sheria ni kutupiana madongo kwenye chombo cha umma kwa kuuchafua umma unatarajia nini???
 
Masanja aache mambo ya kitoto,yote maisha na wala pesa haina mwisho hata uwe tajiri vipi.
Kama alishindwa ITV atulize boli afanye kazi na si ushambenga tuuuuuuuuuu.
 
Kama ni kupiga vijembe watu maarufu mbona walianza tokea wako EATV? Au ndio tunawaona sasa?
 
Sioni kama hawa Orijino Comedy wanakwenda vizuri siku hizi. Tangu wametoka EATV wanapiga majungu tu. hata huko kuchekesha hakuna. Nawaona huko mbele hawatakuwa na mwisho mzuri.

Si hilo la juzi tu. hata week kama mbili kabla waliimba wimbo wakimkashifu Mengi, baadhi ya Maneno ya wimbo huo yalikuwa hivi,

".. Ningetoa mali zangu,, kuwalisha masikini,.... kama sinao upendo... mimi si kitu kabisa..."
Sifai Mbele za Bwana.... Sifai Mbele za Bwana,,, kama sinao Upendo Mimi si kitu kabisa,,,,
huku Masanja akiongezea baadhi ya maneno kama "na vilema na viwete". Akimaanisha Mengi analisha Maskini, Vilema Na Viwete wakati hana upendo.

Lets wait and see mwisho wa haya yote.
 


Once you know they are stupid, jus leave them as they are! Their destiny us ful of shame. I can assure you
 
kila siku wanatupunguzia hamu ya kuendelea kuangalia Ze Komedy
 
be cool men hayo mambo ya kutiana adabu ni mambo ya komedi zote duniani. Uharibifu wa utandawazi yep no ukweli wa mambo yes kabisaaaa lakini nanbi anamjua Mengi kisawasawa. kisha kwanini watu wanakuwa pissed off very izi. kama kucharazwa mtu kalamu si unakaa na domo lililojaa hasira na matrusi yalifungwa zip. Hii dunia huru bana kwe kwe kwe kumbe huuma ehe ehe
 
Sio masanja tu, bali pamoja na washirika na washabiki wake wote IQ zao ni finyu sana.

Hizi kauli ndio uwa sizipendi. Inaonyesha wewe mwenye IQ ndogo pia. Yeye kamkashfu mengi indirect bila kumtaja jina. Alichofanya ni uupuzi na vitu kama hivi vinaweza kumletea matatizo.

Kwa upande wingine wale ni watu wa comedy kuna wakati wanatoa comedy nzuri tu na kupata washabiki wengi.. Sasa unapokuja na kusema washabiki wao IQ zao ni finyu unaweza kukuta mshabiki mkubwa wa masanja ni MAMA yako sasa hapo sijui inakuwaje?

Kuwa makini kabla ya kuandika kitu....Unaboa


Regards
 
kwani hawa wameajiriwa na nani? hebu kwanza tutazame data zetu vizuri. Wameajiriwa na nani? wana kampuni yao hawa walichofanya wameingia mkataba na TBC .Sasa nani hasa ana matatizo? Mbona tunafurahia sana methali ya kiswahili samaki mmoja akioza katika tenga wote wameoza. Msitie kabali isiyopimwa katika mizani unaweza kuwa unajaribu kumtemu papa na ndoana ya tuna. Utachekesha
 
Kiongozi umeona senksi niliyokukabidhi kwa hii yuzifuli posti?
You have said it. You have said it well.
Nadhani mjadala umeuhitimisha vizuri.
Kwamba The Orijino komedy Hawana adabu, waoga na hawana shukrani: Period!
Mjadala haujahitimishwa hata kidogo. Unaposema watu wanakosa shukurani unamaana gani.Yaani kwa kuwa hawa CCM (enzi hizo Tanu) imeleta uhuru basi wao waendelee kuwapo tu hata kama wanaboronga? kila mtu anastahili kufanyakazi zake nashukurani si ya kusubiriwa.Hivi mnajua hasa dhuluma maana yake nini?kukosa shukurani si dhuluma bali kuomba upewe shukurani kwa kosa lililohitimisha dharuba ya mwisho katika ncha ya sindano ndio dhuluma yenyewe.Mwenye masikio huambiwa asikie na mwenye macho aambiwa aone na ambaye hana macho lazima atembee afungue hisia namba sita au la kama ni mchonga vinyago kipofu kupapasa kunaweza kukuletea jibu zuri.Acheni hizo hakuna anayemjua mengi vizuri zaidi kama aliyeshawahi kuingia mkataba naye.Sisi kwetu vicheko na zaburi tu, kila kitu kityalipwa hapa hapa.Unadhani kesi za wafanyakazi wale wanahangaika ni za bure tchao mwenye hasira aropoke mpaka nyongo
 
Jamani Masanja simlaumu sana na siwezi kukubaliana na mtu akisema Masanja ni mlopokaji. Hivi mtu anayesoma taarifa ya habari anaweza kuwa ni mlopokaji? Sasa msi - mjaji Masanja kwa hilo, ila kwa kifupi waandaaji wa kipindi cha the commedy ndo wamekiharibu na kama business world watu lazima watumie weakness zako kutoka hapo sio kosa la EATV. Wakati the comedy ikiwa EATV ukweli mbaya hata mimi nilikuwa naangalia sasa walipohamia huku, du ukikaa na mwanao mtajikuta mnavuliwa nguo maana wanafurahisha aina furani ya jamii na sio mlengo kwa jamii yote. Hivyo tuwaache watakuwa fundisho kwa wengine watakaposhindwa kulipia bill TBC. Maana watakosa watu kabisa, ukipata cheza nacho vizuri usijisahau, sasa wale walijua ndo wenyewe wenye kuweza. haya weee.

Pia mimi nimeona watu wenye access na media mara nyingi huwa wana mis-use, mwangalieni Kibonde clouds anaweza akaanza ku-judge kitu ambacho hana data na kumharibia mtu mambo yake maana kuna watu wanasikiliaza na kuamini period ! hawaendi in details. Lakini jambo ambalo hawajalijua ni adhabu za kificho, they create enemies.
 
you should 1st know what is the so called COMEDY?? na madhumuni yake.....
......then mie sijawahi angalia hicho kipindi sababu nipo mbali na nje ya nyumbani Tz......BUT i'm sure kabisa huyo mchekeshaji hakutaja jina uliloliandika hapo.......
..(kama vp tutafutie hiyo video utuwekee hapa na kututhibitishia akilitaja hilo jina la ulilolitaja wewe hapo juu).....
....USHAURI...usipende tafsiri kauli za watu in negative attitudes bila kujua ukweli halisi wa msemaji binafsi alimaanisha nini .....then kumbuka THAT IS A COMEDY...
 
Big Up Hofstede na Kiranga. kikubwa hapa ni kutoa lugha ya kashfa iwe kwa mtoto hata mkubwa.Binafsi siipendi regardless hiyo lugha inatolewa kwa Ndg.Mengi or ndg Machache . Ila hilo jina la Mengi hatujasikia likitajwa mwanzo hadi mwisho wa kipindi.mwenzetu pakajimmy mmh! ni feelings zako na BROOKLYN au?
 
BABA umesema mwenyewe kuwa huwa hutazami kipindi hicho, kwa jinsi masanja alivyo present kile kipindi huhitaji akutajie jina ili ujuwe mlengwa ni nani? yes wakati wako EATV kipindi kile likiwa COMEDY lakini sasa nafikiri ni zaidi ya komedi. Si mmakumbuka walipoanza kuwasema watu waziwazi katika ile session yao ya ALYEFULIA! tuliposema sana wameondoa! tatizo la crew nzima ya Orijino Komedi ni wapenda visasi sana. Hebu niulize kuna connection gani kati ya MANJI na Orijino Komedi, isije kuwa hawa vijana wanatumiwa tu na "washindani" kama sio wapinzani wa mzee Mengi! BABA nakushauri tu kabla hujaanza kumtetea sana Masanja jaribu kufuatilia historia ya kundi hili!
 
Nilitazama hicho kipindi tangu mwanzo hadi mwisho sikusikia jina la Mengi likitajwa.


Hahah mama mkwe unanitia aibu, sasa kweli wewe hukusikia jina la Mengi na ulitazama kipindi mpaka mwisho. Sasa mkweo muongo basi. Pole
 
massanja hajaenda shule...lete thread za kujadili watu wa maana..ni mpuuzi yule..achana nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…