Masasi: Mfululizo mauaji ya kikatili kwa Wanawake, Polisi wataja wivu wa kimapenzi

Masasi: Mfululizo mauaji ya kikatili kwa Wanawake, Polisi wataja wivu wa kimapenzi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kufuatia mfululizo wa mauaji ya kikatili hasa kwa Wanawake Wilayani Masasi Mkoani Mtwara, Jeshi la Polisi limedai kuwa vyanzo vingi ni masuala ya mapenzi.

Kauli hiyo imetolewa baada ya tukio lingine la mauaji kutokea usiku wa kuamkia jana Agosti 11, 2022, ambapo mwalimu wa Shule ya Msingi Mbaju alikutwa ameuawa na mwili wake kutupwa kando ya barabara.

Msemaji wa Polisi, SACP David Misime amesema kuanzia Machi 2022 kuna mauaji nane na Polisi wanaendelea na jitihada za kuwatafuta wahusika.

Chanzo: Azam TV
 
Inasikitisha
Pole yao wafiwa.
 
Back
Top Bottom