Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) iliyokutana leo Jumanne, Mei 5, 2026 Kinondoni jijini Dar es Salaam imemteua Daudi Masasi kuwa mgombea ubunge wa Isimani mkoani Iringa.
Uchaguzi mdogo wa Isimani utafanyika Juni 1, 2026 kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wake kwa miaka 31, William Lukuvi baada ya kufariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.
Aprili 20, 2026 Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), ilitangaza uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo hilo utakaokwenda sambamba na uchaguzi wa udiwani katika kata 12 za Tanzania Bara utakaofanyika Juni 1, 2026.
Soma Pia:
Masasi atachuana na wagombea wa vyama vingine kikiwemo Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimekwisha kumteua Emmanuela Mtafikolo kwenye mbio hizo.