ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Hongera Waziri Bashe.Hakuna kuchekeana Wala kuoneana huruma kwa mafisadi wote bila kujalisha hadhi Yao.
My Take: Wakulima ungeni mkono juhudi za Waziri Bashe kupambana kuinua Kilimo.
Kazi iendelee,ajenda 10/30.
---------------
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ametoa agizo la kushikiliwa kwa diwani wa Chiwale (CCM), wilayani Masasi, Yusuph Mataula ili kusaidia uchunguzi katika sakata la ubadhirifu wa shilingi milioni 139.
Waziri Bashe ametoa maagizo hayo wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Chiwale wilayani Masasi, Mtwara, baada ya kusikiliza kero mbalimbali zinazoathiri maendeleo ya kilimo katika kijiji hicho.
Katika mkutano huo, Bashe alifahamishwa kuwa baadhi ya wakulima wa korosho ambao ni wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nanyindwa AMCOS hawakulipwa kiasi cha shilingi milioni 139 katika msimu wa 2016/17 hatua iliyosababisha mali za AMCOS hiyo ikiwemo trekta na lori kupigwa mnada kwa amri ya mahakama.
Pia, soma: Naibu Waziri Bashe aagiza TAKUKURU kuanza uchunguzi upotevu wa milioni 150 za AMCOS ya Chabuma