Hiyo ndiyo kauli ya msemaji wa Ruvu shooting akijitetea dhidi ya kauli yake ya jana baada ya mechi ya yanga kwamba kwenye timu kuna"Yuda" Kauli ambayo ilitafsiriwa kama kuna msaliti kwenye timu.
Nimejikuta nacheka peke yangu baada ya kusikia utetezi wake.
Hata hivyo sisi pia watazamaji tuliona kuna kitu si bure.Wachezaji walikuwa wakitoa pasi kwa mpinzani ili afunge goli jingine hasa waliposawazisha kwa bahati mbaya.
Yuda hakufurahia na hiyo akafanya kila liwezekanalo ili waruhusu goli.