silent lion
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,278
- 1,794
Mheshimiwa najua una majukumu mengi ya kitaifa kwa vile wewe ni Waziri, lakini angalau ungezungumza na muwakilishi Mheshimiwa Jazira, mkalipatia ufumbuzi tatizo hili.
Majimbo ya Zanzibar ni madogo mno kulinganisha na bara, yaani huku jimbo unaweza kutembea kwa miguu nusu saa tu ukawa ushalimaliza. Lakini jimbo hilo lina muwakilishi, lina mbunge, lina diwani zaidi ya mmoja, lina sheha zaidi ya moja, cha ajabu wote hawa huwaoni mpaka uchaguzi ukaribie, si vizuri mnavofanya.
Taswira za watoto wadogo wakiwa na ndoo za maji kichwani, pamoja na wakina mama hazipendezi kwa kweli.