Masauni: Muungano Ni Alama ya Tanzania, Usichezewe

Masauni: Muungano Ni Alama ya Tanzania, Usichezewe

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
463ba1e8-8b27-4950-a947-de64c23e8d7d.jpg

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema, kati ya jambo ambalo halipaswi kuchezewa ni Muungano ambao unatakiwa kulindwa na kila mmoja maana ndio alama kubwa ya Tanzania.

Waziri Masauni ameyasema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Julai 22, 2026 akieleza kufurahishwa na shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani zinazofanyika ambazo zinaunganisha na Zanzibar ikiwemo bandari.

"Fursa ya Muungano inatakiwa kusaidia pande zote bara na Zanzibar na katika hili itakuwa inasaidia zaidi kwenye sekta ya utalii kwani mtalii anapokuja Zanzibar anaunganisha na Bagamoyo kwenye hifadhi ya Saadani," amesema.

b858c370-7e8e-45c2-add6-7c50e4fa5867.jpg
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akielezea jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni aliyoifanya Chalinze mkoani Pwani, Julai 22, 2026.

Kadhalika amewataka vijana kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii katika kipindi hiki cha utandawazi kutokana na kuwepo kwa upotoshaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya vijana.

Amewataka kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo ambayo yatakuwa na faida kwao hususani kujifunza mbinu za kuboresha shughuli zao za kibiashara za kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amesema Chalinzi inabadilika kwa kasi kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Ameongeza kuwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi imesaidia kufanya kimbilio kwa wawekezaji wengi kutokana na kuwepo kwa miundombinu Rafiki jambo ambalo limeifanya Chalinze kukua kukua kila siku.


4686c156-fbbc-40cd-a54c-295ef3c291a0.jpg
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (kushoto) akiambatana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge wakikagua ujenzi wa nyumba ya walimu Shule ya Sekondari Matimbwa iliyoko Halmashauri ya Mji Bagamoyo wakati akiwa kwenye ziara wilayani humo, Julai 22, 2026.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alisema Wilaya ya Bagamoyo ni kati ya maeneo ya utalii ambayo kwasasa yanakuwa kwa kasi kwa kuwa na wawekezaji wengi wazawa na wageni wanaofika kuwekeza.

“Kuhusu suala la Muungano hapa Pwani watu wengi wanakutana na kufanya shighuli mbalimbali kutoka Zanzibar na Bagamoyo ni moja ya mji ambao wananchi wananufaika na Muungano wa nchi yetu,” amesema.

8b5b7f11-8b6b-4f0b-9b88-60a99bd3213c.jpg

​
 
Back
Top Bottom