Mr-Njombe
Member
- Aug 29, 2022
- 64
- 122
Wana JF
Kumekua na maoni, mitazamo, mapendekezo na wito kutoka kwa watu mbalimbali mashuhuri, taasisi na vyama vya kisiasa kumtaka waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ajiuzulu nafasi yake, lakini pia hata mkuu wa Jeshi la Polisi nchini nae kufanya vivyo hivyo kulingana na changamoto za kiusalama zinazoendelea nchini.
Kwa maoni yangu, hilo halitaweza kutokea kwa sasa au kufanyika kwa wakati huu, kwani kwa kufanya hivyo ni kuthibitisha uzembe na ushiriki wao katika hayo yaliyotokea, ili hali bado haijathibitika dhahiri kama ni vyombo vya ulinzi ndivyo vinahusika au la. Hivyo kesi hii ya sasa ni tofauti kidogo na ile ya wakati wa Hayati mzee Mwinyi, kwani angalau kipindi cha Mwinyi ilikua bayana kua polisi walihusika kwa namna moja au nyingine.
Ila kwenye hili la sasa, mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja usio na shaka, bali ni hisia na mihemko binafsi ya wananchi, kitu ambacho sio kibaya na ni haki. Hivyo tusitegemee yeyote kujiuzulu labda Mama abadilishe tu mkeka, kuimarisha utendaji wa serikali yake.
Soma Pia:
Mwaveja sana, kwa maoni yako unadhani itaashiria nini au itatoa picha gani?

- Lema: Nilitegemea mpaka sasa baada ya statement ya Rais Samia kuhusu mauaji ya Ally Kibao basi Waziri Masauni, IGP wawe wamejiuzulu
- Tafrani yazuka msibani Tanga: Waombolezaji wakataa dua ya Waziri Masauni wakimtaka ajiuzulu