Elections 2010 Masha adondoshwa Jimbo la Nyamagana; Wenje (Chadema) ashinda

Elections 2010 Masha adondoshwa Jimbo la Nyamagana; Wenje (Chadema) ashinda

Status
Not open for further replies.
jamani nashukuru sana kwa wote mnatuletea hizi habari ila tufuatilie sana kwa umakini maana haya tuliyo nayo ni kiasi kidogo sana kuanza kujiamini kwamba ushindi tayari.

Tuuimizane tupige simu, tutumie internet kufuatilia kila sehemu ili iwe rahisi zaidi maana ni sehemu nyingi sana na kweli hatuwezi kuanza sherekea ushindi. Labda kwa kulinganisha na 2005 hali inaweza kuwa nzuri zaidi maana chadema kwenye urahisi walifikisha kura 600 tu. Kwa hiyo jamani tujitolee wote tufuatilie kila sehemu kama wewe ni wa bukoba tafuta watu kama kumi waliopo uko wakupe matokea, wa songea, mbeya, mtwara na kwingineko tufanye hivyo....ndugu zangu nawaomba sana....natamani sana ushindi lakini mafisadi nao wanafanya kila mbinu kupindua mambo...
 
Mkoa wa Mwanza
Nyamagana
Kituo cha hesawa

Wenje 126
Masha 78

Kituo cha BOT

Wenje 111
Masha 71

Kituo cha Kauma
Wenje 135
Masha 38

Kituo cha saa nane
Wenje 120
Masha 30
 
Kwa taarifa nyepesi toka mwanza nyamagana- masha wa ccm yuko hoi bin taabani mbele ya mgombea wa chadema kwa mbali sana. Karibu sehemu zote za udiwani chadema washachukuwa ushindi tayari. Pia ilemela dialo yuko kwenye intesive care unit, chadema inaongoza kwa juu sana. Hivyo mwanza wamempeleka slaa ikulu.

Kuna mtangazaji kutoka Mwanza Channel 10 , anatoa matokeo ya wali Mwanza , mwanzoni alikuwa anauma uma kusema , mwisho lakini ikabidi aseme tu Wenje yuko juu, matokeo kamili bado...
Wimbo ni wamebana wameachia!!!!
 
Kwa taarifa nyepesi toka mwanza nyamagana- masha wa ccm yuko hoi bin taabani mbele ya mgombea wa chadema kwa mbali sana. Karibu sehemu zote za udiwani chadema washachukuwa ushindi tayari. Pia ilemela dialo yuko kwenye intesive care unit, chadema inaongoza kwa juu sana. Hivyo mwanza wamempeleka slaa ikulu.

Khe khe khe ushikaji unaporomoka kila mtu na lwake .... ... Masha na ngebe zake ati waziri wa mambo ya ndani .... .... ... utauota tu sasa. Huyu ndiye walikuwa wanamtumia kuamrisha askari kutetea mafisadi.
 
Haya arudi marekani! Hivi yule sijui ndo mdogo wake aliyekuwa mjeshi yuko wapi?
 
safi kabisa hayo ndo mapindui ya kweli pindua mafisadi wote
 
wamfariji jamaa kwenye viti maalumu, hivi si ndiye yule aliyehusihwa kwenye deep green au?
 
Nadhani hapo Nyamagana kuna vituo vingi hivyo tueleze hali katika vituo vingine.
 
Vipi Nchimbi jamani?

Songea Mjini wamkalia kooni Nchimbi


picture-34.jpg

Na Gideon Mwakanosya - Imechapwa 27 January 2010

nchimbi.jpg



JIMBO la Songea Mjini ni miongoni mwa majimbo sita ya uchaguzi yaliyopo katika Mkoa wa Ruvuma. Emmanuel John Nchimbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye mbunge wake.
Baadhi ya wananchi wanaoishi katika kata za Mshangano, Namanditi, Ruhuwiko, Mletele, Lizaboni na Msamala katika jimbo hili, wanazungumzia namna walivyosahaulika kutatuliwa kero nyingi katika huduma za maji, umeme na afya.
Wananchi mbalimbali wamemweleza mwandishi wa makala hii, kwamba mbunge wao hajatekeleza nyingi ya ahadi alizoahidi wakati wa kampeni. Mmoja wao anayeishi kata ya Mshangano, Samson Komba, anasema tangu Nchimbi alipochaguliwa, amewatembelea mara chache.
Hamza Uonjo, mkazi mwingine, anasema, "Kwa kweli tumechoka huyu mbunge ameshindwa kututatulia kero ya maji, umeme na upungufu wa wahudumu na vifaa katika kituo cha afya cha Mjimwema. Pia hajaitisha mkutano na wananchi tangu achaguliwe.
Mwandishi ameshuhudia upungufu wa wahudumu, dawa, vitandaa na vifaa tiba mbalimbali katika Kituo cha Afya cha Mjimwema. Kituo hicho pia hakina umeme wa uhakika.
Daktari alikutwa akimkadiria mgonjwa homa kulingana na maelezo ya mgonjwa na akapewa dawa bila ya kufanyiwa kipimo chochote. Umeme ilielezwa kuwa ndio tatizo.
Tatizo la maji limepungua kidogo isipokuwa maeneo ya pembezoni mwa jimbo katika kata za Ruhuwiko, Subira, Mletele, Lizaboni, Msamala na Mshangano ambako bado maji ni shida.
Zuhura Hamidu, mkazi wa Mletele, anasema huamka saa 11 alfajiri kwenda kusaka maji yaliyoko umbali wa zaidi ya kilomita mbili. "Hii hali inatuletea adha kubwa kiafya na inatupotezea muda mwingi ambao tungeutumia kwa shughuli za maendeleo."
Tatizo la umeme jimboni linaelezwa vizuri na mkazi wake, Ally Swai, ambaye ni fundi wa kuchomea, ambaye anasema umeme katika manispaa ya Songea umekuwa ukikatika mara kwa mara.
Upungufu huo unasababisha kuzorota kwa shughuli za uzalishaji na biashara na hivyo kudhoofisha mapato ya wananchi ambao baadhi yao wanapata hasara kutokana na vitu mbalimbali vinavyotumia umeme kuungua.
Hali kwenye Soko Kuu la mjini Songea inaleta malalamiko. Wachuuzi wanalalamikia kitendo cha baadhi ya madiwani kuhodhi vibanda vya kufanyia biashara na kuvipangisha kwa gharama kubwa.
Mbunge Nchimbi anasema anatambua malalamiko ya wachuuzi na ameelekeza idara husika katika manispaa wafuatilie madai yanayotolewa ili utaratibu uliopangwa ufuatwe na kutendea watu haki.
Kwenye afya anasema hali ni tofauti kuliko aliyoikuta miaka mitatu iliyopita na "jitihada zaidi zinaendelea kwa kuboresha kituo cha afya cha Mjimwema na kujenga vituo vipya kila kata."
Kuhusu tatizo la maji, Nchimbi anasema upatikanaji wake hauridhishi lakini amejipanga kusaidia kurekebisha kasoro zilizopo na tayari amepata ufadhili kutoka serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la misaada la KFW utakaosaidia kujenga miradi ya maji kwenye maeneo yasiyokuwa na huduma hiyo.
Nchimbi anahitimisha maelezo yake kwa kusihi wapiga kura wake wamvumilie kwani amekuta matatizo mengi jimboni na amekuwa akichukua hatua mbalimbali kuyapatia ufumbuzi. Kimya chake bungeni anasema kisichukuliwe kuwa hatekelezi ahadi zake kwa wapiga kura.
 
Wamechakachua matangazo ya ITV mtangazaji alipkuwa anatoa Data wamekata matangazo wanaogopa kuaibika. Inaonekana Mwanza ni issue huko
 

... Kweli wachana na nguvu ya Utu wa mtu...

.... Ufisadi is nothing when it comes to peoples power!!

Watanzania ni umoja ktika utu na ubinaadamu wetu...ndio nguzo ya umoja na ujenzi wa Taifa imara lenye heshima ndani na Nje ya Nchi!!

Ufisadi ni unyama , nguvu ya kutugawanya, kututenga...na kutukosesha kuheshimika kama Tz!
 
Masha anazadhania bongo hatuna akili. wananchi ni waelewa. Hapa sio kwa OBAMA
 
Swala si Masha kushindwa ubunge. Ni kashifa ya Deep Green na vitambulisho vya taifa. Maskin atajificha wapi? Mungu mkubwa. Mie nitaanga kwa kuvunja miwan yake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom