Mojawapo ya mafunzo makubwa kabisa katika chaguzi za karibuni za Ulaya ni kwamba kwa raia wengi wa bara hilo Urusi bado sio nchi muhimu kwao na haina uwezo wa kushawishi kupendwa ndani ya nchi nyingi za Ulaya kama viongozi wake walevi na mashabiki wake wengi walivyokuwa wanajiaminisha.
Wakati uvamaizi wa Urusi huko Ukraine unaanza viongozi walevi wa Urusi na wafuasi wake walizilaani sana serikali za nchi za Magharibi na hasa za Ulaya kwa kuiwekea vikwazo na kuitenga huku wakiamini matokeo yatakuwa kwa serikali za nchi hiyo kupoteza madaraka kwa viongozi wapya wenye mahaba au kuegemea Urusi.
Ni kweli tangu vita hiyo ianze kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya uongozi Ulaya katika nchi za Italia, Hispania, Uingereza na Ufaransa lakini kwa raia kuziingiza madarakani serikali na viongozi ambao wako hasi na wenye msimamo mkali zaidi dhidi ya Urusi kuliko wale wa awali.
Hata huko Marekani suala kubwa kwenye uchaguzi wa nchi hiyo sio Marekani kuiunga mkono Ukraine dhidi ya Urusi bali umri wa Biden na skendo za Trump.
Ni wakati wa Urusi na wafuasi wake kukubali tu kwamba kutokubalika kwa Urusi ulaya sio suala la propaganda au MSM kama walivyokuwa wanajiaminisha bali ni uhalisia.