JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Bondia Tyson Fury amefanikiwa kutetea Mkanda wa WBC The Ring baada ya kumpiga Dillian Whyte kwa TKO katika raundi ya sita ya pambano lao la usito wa juu usiku wa kuamkia leo Aprili 24, 2022.
Mashabiki 94,000 waliweka rekodi ya kuujaza Uwanja wa Wembley Jijini London kushuhudia Mwingereza huyo akiutawala mchezo huo kwa raundi nyingi kabla ya kushinda.
Kwa ushindi huo, Fury sasa amepigana mapambano 33, ameshinda 32, ushindi wa KO (23), sare 1 na hajapoteza pambano lolote.
Source: DailMail