Mashabiki na wanachama wa simba Matumaini yao makubwa wameyaweka kwa Al hilal kumtoa yanga

Mashabiki na wanachama wa simba Matumaini yao makubwa wameyaweka kwa Al hilal kumtoa yanga

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Ni wazi kwamba mashabiki na wanachama wa simba wameweka matumaini makubwa kwa Kuisifia Al hilal jinsi itakavyomtoa yanga na wanakwenda mbali zaidi kuapa ya kwamba ndo mwisho wa yanga awatoboi, lakini nafikiri wasichokijua hii ni yanga ambayo aijaingia kwenye hii michuano kwa kubahatisha, yanga imeingia ikiwa imefanya usajili bora, yanga imeingia ikiwa imejipanga ipasavyo ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Yanga imeingia ikiwa inacheza kitimu zaidi inao muunganiko ambao inaweza kucheza mpira na kupata matokeo kwenye uwanja wowote ule aijalishi anacheza nyumbani ama ugenini, Inae kocha makini na bora kwenye mambo ya kiufundi, imejipanga kiuchumi na fitna zote inazijua, kwaiyo anayejidanganya kwa yaliyokuwa yanatokea nyuma akafikiria yatatokea tena safari hii atalia na kusaga meno maana wengi wanafikilia kila siku ni jumapili kwamba yaliyotokea uko nyuma ndo yale yale yataendelea kutokea na ndio maana mashabiki wa simba wanajua ya kuwa Al hilal itaitoa yanga kirahisi rahisi tu.

Muda ni suala nyeti sana na majibu yatapatikana trh 8/10/2022
 
wazi kwamba mashabiki na wanachama wa simba wameweka matumaini makubwa kwa Kuisifia Al hilal jinsi itakavyomtoa yanga na wanakwenda mbali zaidi kuapa ya kwamba ndo mwisho wa yanga awatoboi...
Sio kweli, hao ni mahasimu wa uongozi wa Sasa wa Yanga sio mashabiki wa Simba.

Mashabiki wa Simba wameweka matumaini kwa timu yao kumtoa Premirio de agosto na kutinga hatua ya makundi.

Hayo ya Yanga wala hawana muda nayo acha kuwazushia uongo.
 
Hakuna shabiki SimbaSc aliyeweka matumaini kwa Hilal, ila kwa yoyote yule mwenye akili ni lazima akubali kuwa kipimo cha mikikimikiki ya CAFCL kwenu nyinyi kinaanzia hatua inayofuata kwasababu ya ushindani mtakao kutana nao.

Cha kufanya ni nyinyi kushinda na kuitoa Al Hilal badala ya kuucheza mpira kwa midomo mirefu na vidole kama hivi.

NB: Kuna yule jamaa mwenye avatar yenye jina linalofanana na la kocha msaidizi wa Simba Sc, hawezi kupita huu uzi bila kuacha tusi maana ni bingwa wa kuucheza mpira kwa mdomo.
 
Nilitaka kushangaa, yani tuwe na matumaini kwenye mechi isiyotuhusu kana kwamba haya mashindano tumeyajua msimu huu?
 
Hakuna shabiki SimbaSc aliyeweka matumaini kwa Hilal, ila kwa yoyote yule mwenye akili ni lazima akubali kuwa kipimo cha mikikimikiki ya CAFCL kwenu nyinyi kinaanzia hatua inayofuata kwasababu ya ushindani mtakao kutana nao.

Cha kufanya ni nyinyi kushinda na kuitoa Al Hilal badala ya kuucheza mpira kwa midomo mirefu na vidole kama hivi.

NB: Kuna yule jamaa mwenye avatar yenye jina linalofanana na la kocha msaidizi wa Simba Sc, hawezi kupita huu uzi bila kuacha tusi maana ni bingwa wa kuucheza mpira kwa mdomo.
Baadaye msije mkasema tena Al Hilal ni timu dhaifu!! Mara oooh.!! Yanga imebahatisha!!

Time will tell.
 
Sio kweli, hao ni mahasimu wa uongozi wa Sasa wa Yanga sio mashabiki wa Simba.

Mashabiki wa Simba wameweka matumaini kwa timu yao kumtoa Premirio de agosto na kutinga hatua ya makundi.

Hayo ya Yanga wala hawana muda nayo acha kuwazushia uongo.
Matumaini ya Simba ni kutinga nusu. Tunapambana na rekodi zetu. Uto wameingia wenyewe cha kike wasitafute wa kumfia
 
Hesabu azisemi uongo kati ya Vipers utd na Al hilal nani yupo juu,kama aliyeko chini kakubamiza vipi yule aliyeko juu atakuacha?.vipi level ya Al hilal na Uto nani yupo juu ya mwenzie?
 
Sio kweli, hao ni mahasimu wa uongozi wa Sasa wa Yanga sio mashabiki wa Simba.

Mashabiki wa Simba wameweka matumaini kwa timu yao kumtoa Premirio de agosto na kutinga hatua ya makundi.

Hayo ya Yanga wala hawana muda nayo acha kuwazushia uongo.
Kumbe OKW BOBAN SUNZU ni mamluki tu sio shabiki wa Simba kindaki kindaki
 
Mashabiki wa simba mnawasingizia tuu. Hatuwezi kutamani Yanga itolewe ilhali mechi si yao. Sisi tunatazama jinsi gani tutapambana na mechi ijayo na kusonga mbele tu.

Sijui kwanini tangu asubuhi na kutana na nyuzi za midomo ya Wana Yanga kuhusu mechi yao ijayo. Jiandaeni vyema Mana mechi itakuwa tamu sana.
 
Usitusemee mimi nina uhakika utopolo itamtoa al hilal
 
Back
Top Bottom