Mashabiki Simba wasimlaumu Aragija bali walaumu Viongozi wao

Mashabiki Simba wasimlaumu Aragija bali walaumu Viongozi wao

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
18,360
Reaction score
26,244
Mechi ya Simba na Azam refa alikuwa Aragija, Simba walikataliwa penati mbili za wazi lakini pamoja na viongozi kulalamika hadharani hawakuchukua hatua yoyote baada ya kamati ya masaa 72 kukaa kimya. Inaonekana viongozi wa Simba hawajui ukubwa wa hii timu kipaumbele chao ni maslahi wanayopata.

Kama wangeshupalia maamuzi mabovu ya huyu kipa ni wazi Aragija asingechezesha tena ligi msimu huu.
Kuendelea kulalamika kwa kitu unachojua kingefanyika ni ujinga wa kiwango cha juu.

1782383446001.png
 
Kutoka kumtegemea azam kuwa ataisimamisha yanga mpaka kuitegemea TRA united,mashabiki wa simba ni vinyonga.
 
Uongozi uliokuwa "serious" ulikuwa ni wa Babra tu. Na kiongozi mwingine "serious" alikuwa mzee Hanspope (RIP). Hawa wengine ni tia maji tia maji tu. Babra aligomea GSM asidhamini ligi na TFF wakaufyata. Nina hakika Babra angekuwa kiongozi hao wakina Damaro, Bada na Keyekeh wasingecheza kama raia badala yake wangecheza kama wageni. Na hata huyo Aragija na beji yake ya CAF angefungiwa na lingekuwa fundisho kwa marefa wote waliokuwa wanacheza na matakeo ya Simba kwenye ligi kuogopa kufanya hivyo. Aragija ndio aliyefanya kosa kubwa lililoigharimu Simba ubingwa hakufungiwa lakini Mabena kosa lake halikubadilisha chochote kwenye nafasi ya Simba kwenye msimamo wa ligi akafungiwa bado viongozi wakaa kimya tu juu ya Aragija.

Uongozi usioweza kufuatilia mambo madogo madogo kwa ukaribu ni ngumu sana kuupata ubingwa wa ligi hii ya ndani iliyojaa kona kona. Kila mwaka itakuwa viongozi wa Simba wanabaki tu na stori kuwa "tumeukosa ubingwa kidogo tu" wakati wenzao Yanga wanabeba kombe hilo kila mwaka. Kwanza ni aibu kubwa sana timu inayoongozwa na bodi yenye watu 10+ kupelekeshwa na vichwa viwili tu pale Yanga (Arafat na Hersi). Ikitokea Simba wamekosa ubingwa na ndio mwelekeo unaonekana utakuwa hivyo inabidi lawama zote ziende kwa uongozi wa Simba na si vinginevyo.

Viongozi wa sasa hivi naona kama wapo kimaslahi binafsi zaidi kuliko maslahi mapana ya Simba. Hata sajili zao za kimagumashi tu. Hebu fikiria Fadlu alimtaka Mligo lakini walivyo majasiri wakampeleka kambini nje ya nchi Miraji Zambo badala yake. Na mwaka huu ni kama wameshaanza michezo yao maana tetesi ya Sopu imeshika kasi wakati mawinga wa maana wa ndani kama idd Nado, Edgar Wiliam na Bakar Msimu wapo. Sasa huyo Sopu wa nini pale Simba? Kwanza sasa hivi Simba haina kabisa upungufu wa mawinga na hasa ikizingatiwa kuwa watasajili washambuliaji wakati wawili/watatu bado Mpanzu atarudi pembeni na kuongeza idadi ya mawinga.

Kubwa kwa mashabiki wa Simba washukuru Mungu ujio wa Barker na sajili zake alizofanya za Toure, Libase na Oura. Vinginevyo Simba mwaka huu ingeshika hata nafasi ya tano. Jambo la muhimu viongozi wamwache huyo kocha afanye sajili zake na wasimwingilie maana kwa mwonekano wake inaonekana huyo hataki ujinga na hachelewi kuwaachia timu yao. Pia viongozi wa Simba wawe "serious" na kufuatilia kila jambo kwa ukaribu bila kudharau kitu chochote hata kikiwa kidogo kiasi gani kwani mwisho wa siku ubingwa ndio hupatikana huko. Na pia wajue ubingwa unapatikana kuanzia mechi ya kwanza ya ligi na sio kusubiria mwishoni eti mtani apoteze pointi.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom