Mashabiki wa Alikiba siyo real, ni maadui wa Diamond – Mama Ashura

Kwanini wanaompenda diamond wanamchukia Ali kiba?
Yaani hawataki hata kusikia nyimbo zake.
Lakini mimi ninayempenda kiba, nina nyimbo zote za mond.
Hizo tafiti uchwara wazipeleke koromije.
 
Amezungumza kitu ambacho kwa akili ya kawaida huwezi kugundua, kwanza kwa ki uhalisia tu Ali Kiba sio wa kumshindanisha na Diamond maana Diamond ameanza Mziki 2009 Ali Kiba kaanza na kina Dully , sheta , Mr Blue kwa mafanikio ya Diamond ndio yameleta chuki na ukichanganya na mashabiki wa Wema ,Joketi , Penny na Ali Kiba wote wameungana kumpiga vita Diamond
 
Kabla ya kiba kurudi kwa njia ya bifu jiulize alikuwa na tuzo ngapi.....ndo uta conclude usemi wa mama ashura

Nikukumbushe tu
Kipindi domo anatoka, katika tuzo za ktma 2010 mond alichukia tuzo 3 mbele ya mchizi wa getto. Mwaka ulofata wote walilamba garasa mwaka huwo 20% ndo alikimbiza. 2012 domo alikula tuzo 2 mbele ya kiba Akiwa hot na single yake ya mapenzi yana_run dunia. 2013 nakumbuka kiba aliambulia tuzo moja ya ngoma yake ya dushelele na nyingne ya kushirikiana kat yake na ommy dimpoz wimbo wa nai nai, domo akaramba tuzo 3.....baada ya happ kiba akaamua kujipumzisha maana upepo ulikata domo alikuwa anampeleka puta akarudi bench kujipanga ndo akarudo 2015 na gia ya beef. So kutokana na analysis yang apo juu inaprove kabisa kuwa kiba anabebwa na beef bila beef hamna kitu pale.
 
Yaani kabisa unaamini Kiba ana mashabiki wengi kuliko Diamond?! Halafu una habari hata hizo tuzo unazosema zina-reflect kile kile ambacho amesema huyo Mama Ashura?!

Au umesahau haters wakiongozwa na Wema pamoja na Jokate walivyokuwa wanapiga kampeni ili Diamond asichukue tuzo?! Ni hao hao haters ambao walikuwa wanakesha kuhakikisha Seduce Me inapata views nyingi! Lakini kwavile ukweli ni kwamba Kiba hana mashabiki wengi walio loyal, ndio maana leo hivi sasa Seduce Me ambayo iliwahi kuizidi Zilipendwa kwa Views laki 9, hivi sasa imezidiwa kwa views zaidi ya laki 2.5 na gap linazidi kupanuka kila kukicha!!!
 
Eti mmeanza kumshabikia kabla ya Domo! Hoja ya kitoto kabisa hii!!! Yaani unashangaa hilo?! Hata ule msemo wa Kiswahili usemao ujanja sio kuwahi bali kupata inaelekea ni msemo uliokupiga chenga!!!

Kabla Michael Jackson hajafahamika kulikuwa na mamia ya wanamuziki wa pop duniani kabla yake lakini hivi sasa ni Michael ndie alikuja kufahamika kama mfalme wa pop!!
 
Watakwambia izo viewz ni kwa sababu kuna watu sita wamehusika kwny wimbo.
 
Hoja ya wanaomshabikia/fan wa kiba ni madui wa diamond ñi mufilisi kabisa kila msanii ana mashabiki wake,mfano mi napenda mziki mzuri huo ujinga sina kabisa.Vipi wale shabiki wa mond wanaomtukana alikiba kila siku kwenye social pages zake ni maadui wa nani?Twende YouTube kwenye wimbo wa alikiba wa seduce me kuna Matusi,maneno ya chuki kwa hii nyimbo vipi wanamchukia diamond? Hata hapa Jf jaribu kufanya kautafiti kati ya Mondi na Kiba nani anaongoza kuwa haters wengi alafu leta mrejesho
 
Kama hilo hulijui basi I doubt kama ni mfuatiliaji wa haya mambo! Ingawaje sio wote wanaomshabikia Kiba ni haters wa Diamond lakini kama ni mfuatiliaji katu huwezi kupinga hoja kwamba kuna watu kibao ambao "wanamshabikia" Kiba ambao kimsingi ni haters tu wa Diamond na majority waliibuka baada ya Wema Sepetu kupigwa chini na Diamond!

Hivi nchi hii ushawahi kusikia kampeni dhidi ya Kiba kwenye tuzo zozote?! What about kampeni dhidi ya Diamond?! Umesahau kwenye tuzo za MTV na KTMA?!
 
Hizo ni conspiracy ambazo hazina maana.Hizi mashabiki wa Mond wanampenda Alikiba?If the answer is yes,Kwanini wanamtukana kila siku?If no,Huoni kuwa unakosea kusema mashabiki wa kiba ni haters wa Diamond?
Vipi waKenya wanaomshabikia Alikiba nao wanamchukia Diamond
 
Kiba ndo alianzisha iyo chuki angerudi na mwana yake kwa aman bila mgongo wa beef na mond sizan hata hizi team kama zingekuwepo, kwanza mziki wa kibongo ulikuwa umekuwa kila msanii alikuwa anatoa wimbo unahiti lkn tokea yaje haya matimu bongo flava inazid kufa tu daily kuna wasanii wakali kabisa lkn hawasikiki kwa sabbu ya huu upuzi.
 
Kuna prove gn kuwa kenya mond hana mashabiki weng kulingana na kiba maana naonaga humu mnajichetua tu wakati hata wakienda wote kupiga show sehem moja mond ndo anakulaga mkwanja mwingi......ebu nipe prove yako kuwa kenya mond hamfikii kiba kimashabiki.
 
Hamueleweki,Mara mashabiki wa Alikiba ni kwasababu ni haters wa Diamond,or Mara Alikiba aliporudi kwenye industry or Walikuwa mashabiki wa Wema.Kauli ipi ni sahihi Mkuu.Maybe nikusaidie wakati Alikiba anarudi kwenye industry Wema na Diamond walikuwa bado in relationship
 
Weka ushahidi kuwa Mond ndo analipwa mkwanja mrefu
 
Kiba bila beef hana kitu mbele ya domo ukubali ukatae but in reality ndo ukwl huwo.....mashabiki wa kiba ni haters wa mond walio weng ndo maana hata ukitaka kupruvu tembelea page zao zimejaa picha za mond kuliko msani wanaemshabikia na ikitokea akatokea msanii mwingne akahiti unaona wanalalia uko kumbuka kipindi cha mziki ya darasa wote walihamia kwa darasa wakawa wanamshindanisha na domo, Kabla ya beef lao mond alikuw anamvuruga kila sector fatilia matamasha tuzo za ktma pote kule kiba alikuwa anachezea coz kulikuwa hakuna tension ya beef lkn baada ya beef tu kuanza kiba aliporudi na plan B ya beef so wote waliokuwa wana chuki na mond wakahamia kwa kiba na ukijumulisha kuvunjika kwa penzi la domo na wema hasira za mashbiki wa wema wakazimalizia kwa kumukomoa mond kumbuka tuzo za ktma kilichotekea 2015.

Ikitokea kuna tamasha wapo kiba na mond utaona mashabiki wa kiba akipanda mond wanaanza kurusha makopo na kuzomea na wakati kiba akipanda mashabiki wa mond huwa hawafanyi huo ujinga wa kurusha makopo na vitu ka izo.

Na hata ikitokea mtu akaamuwa kuwapatanisha mond yupo tyari wakae chini yaishe coz kwake beef halina faida lakin kiba hawezi kukubali na Piga uwa garagaza hawezi kukubali maana likiisha tu beef msoto unaanza.

Izo no prove tosha kuonyesha kuwa watu wanaomshabikia kiba percentage kubwa ni watu wenye chuki na mond.
 
Mashabiki wa diamond ndo wanamchukia kiba kwasababu ni wabinafsi kama msanii wao yaani hawataki asikike msanii mwingine ispokuwa domo... Yaani huu ni upumbavu wa kiwango cha lami
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…