Mashabiki wa Alnasr wamshukia Cristiano Ronaldo wamtaka kocha ampige benchi kutokana na kiwango duni uwanjani

Dah ila ronaldo sjui ana kamkosi yule mwamba???
Kuna watu mnafikirisha sana ! sijui ni umri au ni ubishi wa asili? The highest paid footballer, top scorer of all time in UCL, internationally, 5× UEFA champions League winner, 5× Balon O Dior . Euro cup, Nation League, England kashinda kila kitu, Spain kaweka records , Seria A kafanya mabalaa Niambie kuna mchezaji gani mwingine unae mjua ana hizo records?
 
Bado anakwambia huyo mtu ana mkosi sasa sijui yeye ambaye hana mikosi kafanya kipi kwenye maisha haya
 
Duniani hukuna mtu mwenye mwezie, ndio maana kila mtu ana kitu tofauti na mwingine! Mwambie huyo mwenzie akachukue Seria A na EPL
Hayo ni makombe yanayo tolewa na mashirikisho ya mpira ya nchi husika, mwambie alete kombe kubwa kuliko makombe yote duniani yaani kombe linalo andaliwa na baba la mashirikisho yote (FIFA) namaanisha kombe la DUNIA ndio tuanze mazungumzo upya.
 
Unachezea al nasry kweli😄 utaachaje kufunga!!

Kwanza ifike mahali muone aibu kumfananisha Goat na ronaldo wenu
 
Hayo ni makombe yanayo tolewa na mashirikisho ya mpira ya nchi husika, mwambie alete kombe kubwa kuliko makombe yote duniani yaani kombe linalo andaliwa na baba la mashirikisho yote (FIFA) namaanisha kombe la DUNIA ndio tuanze mazungumzo upya.
Worldcup sio kipimo cha kua mchezaji bora, kama ni hivyo basi Giroud ni bora kuliko Lewandosky
 
Hahahaaa!! Umri 38 years. Wanataka kiwango gani.
 
Huyo kijana Mreno kashapoteza sifa ya kulinganishwa na Lionel Andunje mzee wa kukusanya kijiji na kukipelekea moto chote na bao juu yaani goli.
Hayo ni maoni yako upo sahihi kulingana na uelewa wako! kama unatumia worldcup SI unit ya uchezaji bora basi Enzo Fernandez ni bora kuliko Luca Modric
 
Kwa Nini Kila siku yeye tu.?
 
Ashinde kombe la dunia kwanza, mwenzie analo tayari.
Mwaka 1995 George Weah alichukua tuzo ya kuwa mchezaji bora duniani, lakini timu yake ya taifa sio tu haikuwahi kuchukua kombe la dunia, bali hata kushiriki michuano ya fainali za kombe hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…