Hili la uboya linawahusu sana wale wa rika langu... ambao huenda hawakuijua Arsenal hadi wapo wavulana wakubwa!
Hivi unaweza kueleza watu hapa ilikuwaje kuwaje na lini ulianza kuwa na mahaba na hii "Saratani ya Moyo?" Hizi Simba na Yanga; sawa tu manake wengi wetu ni timu za kurithi kama tulivyorithi dini na makabila! Hadi tunapata akili; tayari tukakuta miiba kenge kooni... ama Yanga au Simba!
Vipi kuhusu Arsenal?! Hivi ukichunguza sana huwezi kugundua ni uboya tu ndio ulipelekea ujidunge mwenyewe hii Saratani ya Moyo?!
Nianze na mimi mwenyewe! Kitambo sana nikiwa Form I au Form II. Nilikuwa shabiki kufa mtu wa Yanga! Europe Nilikuwa naipenda sana AC Millan!
UK nilikuwa nazifahamu timu kadhaa lakini Arsenal haikuwa moja wapo! Nilikuwa naichukia Liverpool kwa sababu enzi hizo Simba walikuwa wanajiita Liverpool ya Msimbazi... kwangu ikawa nongwa na nongwa ile nahisi nitaingia nayo kaburini!
Narudia; Arsenal nilikuwa siifahamu! Jezi za Man U ikawa ni nongwa yangu nyingine!
So, kwa timu kubwa 2 za UK, sikuwa shabiki wa yeyote... labda niseme nongwa yangu kwa Simba ikanifanya nizichukie BIG 2 za UK!
KUJIDUNGA KIMETA CHA SARATANI YA MOYO!
Ilikuwa Jumamosi... sikumbuki mwezi wala tarehe lakini nilikuwa ama Form I au Form II.
Nikiwa naelekea Taifa (Uwanja wa), pale maeneo ya Uwanja wa Ndani nikaokota kipande cha gazeti! Sijui kama Ilikuwa ni kipande cha gazeti la Uhuru, Mzalendo au Mfanyakazi!
Sina uhakika ikiwa hata gazeti la Majira lilikuwepo enzi zile! Hii ni kuelekea miaka ya 90 katikati!
Basi bwana! Kwenye kipande kile cha gazeti kulikuwa na habari kuhusu timu moja ya Ligi Kuu ya Uingereza! Habari ikaendelea kusema kwamba timu ile eti ina undugu na Yanga ya Jangwani! Kwamba, muda si mrefu Yanga itakwea pipa kwenda UK kukutana na "dada" yake timu ya UK!
Timu hiyo si nyingine bali ni ARSENAL!!
Popote pale ulipo Mwandishi ambae uliandika ile "habari", God is Watching You!
Remember bado nilikuwa mdogo! Kwa umri wangu habari ile nikaimeza na kushushia na maji baridi kama ilivyo! Nikaichukua ile sindano yenye Kimeta cha Saratani ya moyo; nikajidunga mimi mwenyewe katikati ya moyo! Fasta sumu ikasambaa mwilini na hadi narudi home tayari nilishakuwa Arsenal Kindakindaki ingawaje sikuwa nafahamu hata rangi ya jezi wanazovaa let alone angalau mchezaji wao mmoja! Wakati ule hata huyu Babu wa Kifaransa mwenye undugu na Mr. Bean alikuwa bado hajaingia Arsenal!
Awali ilikuwa ngumu kidogo kufuatilia ligi kuu ya UK manake njia pekee ilikuwa ni radio!
Miaka michache baadae yule Babu akaja Arsenal! Na kipindi anaingia tayari ilikuwa rahisi kufuatilia Ligi Kuu ya UK manake tv zilishaenea... anyway, angalau home tayari tulishakuwa na TV!
Basi bwana... miaka ya awali Babu yule akawa ananipa raha kweli kweli kupitia hii Timu Dada ya Jangwani!
He! Miaka kadhaa baadae mambo PINDU PINDU! Kabla ya kukaa mbele ya tv kuangalia mechi ya Arsenal; natafuta kwanza Asprin za kuniwezesha kuangalia mechi kwa dakika 90 na Piriton zangu pembeni za kubugia baada ya mechi ili kutafuta usingizi!
Miaka nenda rudi maumivu! Saratani ikautafuna moyo ikaanza kushambulia ubongo! Wakati natafuta kinga saratani isienee kwenye ubongo; 8 hizi hapa!!
Hapo nilishakuwa mtu mzima na miaka mingi ilishapita ! Nikajiuliza hivi hii Saratani nimeipatapata vipi!
Nikakumbuka kipande cha gazeti pale taifa enzi hizo nikiwa kavulana! Nikajiuliza kwanini yule Mwandishi aliamua kugawa ile dozi! Sikupata jibu lakini nikahisi huenda ilikuwa ni kwa ajili ya Siku ya Wajinga!
Enzi zile Siku ya Wajinga haikuwa maarufu kwahiyo ilikuwa rahisi sana kulisha watu matango pori hususani kama unatumia gazeti!
Nikasema ebo! Kumbe inawezekana kabisa hii saratani nimejidunga kutokana na ujinga wangu!! Kumbe mahaba yenyewe haya yametokana na kuuziwa mbuzi kwenye gunia... si sawa na ndoa ya mkeka hii!!
Btw, kwanini niendelee kuwa mjinga huku nikiruhusu saratani ienee kwenye moyo!
Taraaatibu, nikaanza kuzipotezea baadhi ya mechi za Arsenal na kufuatilia tu matokeo yake! Ikafika wakati sina time hata na usajiri wao! Ukikuta naangalia mechi yao basi ni accident tu!
Saratani imepona kwa 90%! Juzi juzi hapa nilikuwa nasikia tu, Sanchez! Sanchez! Hivi kaongeza Mkataba; au? Hivi Ozil bado yupo huko?
Hivi sasa nimeikumbuka Arsenal baada ya kuona video clip kwenye Instagram Account ya Haji Manara ikionesha fara mmoja huko Kenya amejitundika kitanzi na jezi yake ya Arsenal! Yaani Kimeenea kwenye moyo, kikaenda kushambulia ubongo hadi jamaa akabaki garasa tu kichwani!
Acheni ufara nyinyi... mtaendelea kufa na kuacha wazazi, wake na watoto zenu!! Tayari tuna vimeta vya urithi vya Simba na Yanga; ya nini kujidunga vimeta vipya?!
Nishaanza kujipendekeza kwa Barca!!