Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Baada ya saga lake la usajili kutikisa hatmaye mshambuliaji wa the Super Eagles, Victor Osimhen amekubali kujiunga na klabu ya Galatasaray kwa mkopo kwa msimu ujao.
Mashabiki wa Galatasaray wameonyesha shangwe na furaha kubwa baada ya kuwasili kwa Osimhen, mshambuliaji mahiri anayetarajiwa kuimarisha kikosi cha timu hiyo. Ujio wake umewafanya mashabiki kujaa mori, wakimkaribisha kwa shangwe na nderemo, huku wakitarajia kuiona timu yao ikifanya vizuri zaidi msimu huu
Liverpool ilikuwa ni moja kati ya timu zilizotaka kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria, Victor Osimhen katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini ilishindikana baada ya kutaka mshahara mkubwa.Mabosi wa Liverpool walitaka kumsajili Osimhen, 25 kujiandaa na maisha bila Mohamed Salah ambaye mkataba unamalizika mwisho wa msimu huu. Salah anahusishwa na timu nyingi za Saudi Arabia tangu majira ya kiangazi 2023.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alikuwa kwenye rada za klabu ya Premier League Chelsea kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la England siku ya Ijumaa, na pia klabu ya Saudi Arabia, sasa ameelekea Istanbul. Osimhen amefunga mabao 76 katika mechi 133 alizochezea Napoli na alikuwa na mchango mkubwa katika ushindi wao wa taji la Serie A msimu wa 2022-23 kwa kufunga mabao 26.
Osimhen amefunga mabao 76 katika mechi 133 na aliongoza Napoli kutwaa taji la Serie A msimu wa 2022-23. Hata hivyo, kiwango chake kilishuka msimu uliopita akifunga mabao 15 pekee. Napoli wamesajili Romelu Lukaku kwa pauni milioni 30, wiki iliyopita kama mbadala wake