Mashabiki wa mpira hoyee, naona sasa hivi mnapumulia juu juu

Mashabiki wa mpira hoyee, naona sasa hivi mnapumulia juu juu

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Poleni na majukumu ndugu zangu.

Mpira una mashabiki maelfu kwa kwa mamia, miongoni mwao mimi sijabahatika kuwemo. Dah alieniroga, hakika sijuwi nimwambieje!

~ Ukiwa na mimi ukaleta habari za mpira kwakweli naona kama vile umekosa la kuzungumza.

~ Kikifika kipindi cha michezo/uchambuzi sijui wa soka, huwa nazima redio, kama TV nabadili channel.

~ Siendi ukumbini kuangalia mpira tofauti na Taifa Stars, hata hivyo sishangiliagi goli, kufunga au kufungwa naona ni kitu cha kawaida sana.

Kwa kipindi hiki ambacho rafiki zangu wapo na heka heka za Kombe la Dunia, mimi nitakuwa mpweke sana!

Je, humu hakuna ndege wa aina yangu ili turuke pamoja?
 
Wewe Ni mwanamke uliyepewa maumbile ya kiume.
Mwanaume Kama huna shobo na mpira wa soka unatakiwa uende ukamwone daktari ukapime afya ya akili yako.
 
Back
Top Bottom