Mashabiki wa Real Madrid wanapomshangilia Iniesta wa Barca katika 'El Clasico'

Mashabiki wa Real Madrid wanapomshangilia Iniesta wa Barca katika 'El Clasico'

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Katika mechi ya 'El Clasico' ya Jana kati ya mahasimu wakubwa Real Madrid na Fc Barcelona tukio kubwa ni lile la mashabiki wa Real Madrid waliposimama na kumshangilia kiungo mahiri wa Fc Barcelona Andres Iniesta wakati alipokuwa anatoka uwanjani dakika 77 kumpisha mchezaji mwenzake kinda Munir El Hadadi.

Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Real Madrid Bernabeu, Barca waliitandika Madrid 4-0.
Hii ni mara ya pili kwa mashabiki wa Real Madrid kushangilia mchezaji wa Barca. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 kwa Ronaldihno katika uwanja huo huo wa Bernabeu ambapo Barca waliichapa Madrid 3-0.

Jana Iniesta alicheza kwa dakika 76, alifunga goli moja 'matata' sana, ali assist moja, dribbles mara 4, pass accuracy 96%. Alicheza katika kiwango cha juu na kuonesha au kuufanya mchezo wa mpira uonekane kama rahisi na yeyote anaweza kuucheza.

Wakati anatoka uwanjani dakika ya 77 mashabiki wa Real Madrid hawakusita kusimama na kumshangilia (Standing Ovation) kwa uwezo mkubwa aliouonesha dhidi ya timu yao. Huyo ndio 'Iniesta Fiesta' au 'IniestaGram'
attachment.php
 

Attachments

  • iniesta.JPG
    iniesta.JPG
    54.6 KB · Views: 1,830
Ndo demokrasia ya mpira hiyo! Eti! Hapa Tanzania Simba Vs Yanga ni uadui, Chadema Vs CCM ni uadui pia. Hatuwezi kuendelea iwe kwenye michezo au kiuchumi, full kuhujumiana tu!
 
Inabidi tuingize kwenye mtaala kabisa!,samaki mkunje angalia mmbichi.
 
Ndo demokrasia ya mpira hiyo! Eti! Hapa Tanzania Simba Vs Yanga ni uadui, Chadema Vs CCM ni uadui pia. Hatuwezi kuendelea iwe kwenye michezo au kiuchumi, full kuhujumiana tu!

Yule Yacine Brahimi wa Algeria anastahili kupewa heshima hiyo maana ndiye katusababishia kipigo cha 7-0.
 
Kuna wachezaji hata kama unawachukia, HAMNA jinsi! Inabidi uwashangilie tu na kuwapa heshima wanayostahili, ndo walichofanya washabiki wa Madrid jana.
 
sio hao tu waliowahi kushangiliwa santiago benabeau wengine ni #del piero+maradona+gaucho+iniesta#.
 
sio hao tu waliowahi kushangiliwa santiago benabeau wengine ni #del piero+maradona+gaucho+iniesta#.
Ni utamaduni mzuri kutambua kazi ya mchezaji uwanjani. Michezo si uadui bali ni Amani na upendo.Mashabiki wa Yanga na Simba tujifunze na kuuiga utamaduni huu katika mechi zetu hasa za watani wa jadi.
 
kibongo bongo wanakurushia chapa za mikoko!
 
Hyo Gaucho alishangiliwa hata stamford Bridge alipowapiga chelsea goal baada ya kukata kiuno

Gaucho ilikua ni lazima hata kama humpendi mpe tu heshima yake.

Alikua anastahili hiyo heshima,sijawahi kuona mcheza mpira kama yeye, alisababisha nikapenda mpira.

Chelsea na morinyo wake hawatamsahau.
 
Back
Top Bottom