poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
Katika mechi ya 'El Clasico' ya Jana kati ya mahasimu wakubwa Real Madrid na Fc Barcelona tukio kubwa ni lile la mashabiki wa Real Madrid waliposimama na kumshangilia kiungo mahiri wa Fc Barcelona Andres Iniesta wakati alipokuwa anatoka uwanjani dakika 77 kumpisha mchezaji mwenzake kinda Munir El Hadadi.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Real Madrid Bernabeu, Barca waliitandika Madrid 4-0.
Hii ni mara ya pili kwa mashabiki wa Real Madrid kushangilia mchezaji wa Barca. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 kwa Ronaldihno katika uwanja huo huo wa Bernabeu ambapo Barca waliichapa Madrid 3-0.
Jana Iniesta alicheza kwa dakika 76, alifunga goli moja 'matata' sana, ali assist moja, dribbles mara 4, pass accuracy 96%. Alicheza katika kiwango cha juu na kuonesha au kuufanya mchezo wa mpira uonekane kama rahisi na yeyote anaweza kuucheza.
Wakati anatoka uwanjani dakika ya 77 mashabiki wa Real Madrid hawakusita kusimama na kumshangilia (Standing Ovation) kwa uwezo mkubwa aliouonesha dhidi ya timu yao. Huyo ndio 'Iniesta Fiesta' au 'IniestaGram'