Mashabiki 18 wa soka wa Senegal waliowekwa jela kwa kosa la kuingia uwanjani wakati wa fainali ya fujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kule Rabat mwezi Januari 2026, wamekana kuhusika na kosa lolote.
Awali Februari 2026, mahakama nchini Morocco iliwahukumu mashabiki hao kifungo cha kuanzia miezi mitatu hadi 12 gerezani kwa makosa ya uhuni (hooliganism). Upande wa mashtaka uliomba adhabu kali zaidi katika mahakama ya rufaa Rabat, lakini siku ya Jumatatu, mahakama iliamua kubaki na hukumu ile ile ya awali.
Wanasenegal hao walijitetea kuwa walilazimika kuingia uwanjani kutokana na msukumo mkubwa wa umati wa watu, ama walikuwa wakijaribu kukwepa kutemewa mate na kurushiwa vitu na mashabiki wengine.
Walisisitiza kuwa hawakuingia uwanjani kupinga uamuzi wa mwamuzi mwishoni mwa fainali hiyo ya AFCON iliyopigwa Januari 18, ambapo Senegal ilishinda 1-0 dhidi ya wenyeji. Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, amepaza sauti na kulaani vikali uamuzi huo wa mahakama.
Soma pia
Chanzo: Al Jazeera

- FT: Senegal 1-0 Morocco | AFCON 2025 | Fainali | Stade Prince Moulay Abdallah | Jan 18, 10:00 PM | Senegal yatwaa Ubingwa
- Senegal wapokwa ubingwa wa AFCON 2025 na CAF, apewa Morocco
Chanzo: Al Jazeera