Mimi ni shabiki wa simba lakini kuna baadhi ya mashabiki wa Sumba wanakera! Ukipitia akaunti nyingi facebook na mitandao mingine ya kijamii, unakuta mashabiki wengi wa simba wanaeneza habari kuwa Asante Kwasi pamoja na Mchezaji mwingine wa Kutoka Msumbiji ( jina limenitoka) Eti wanatua simba na taratibu zimekamili, ilihali wachezaji wenyewe pamoja na timu wanazocheza kwa sasa wanakanusha Mara kwa Mara uvumi huo, lakini Mashabiki wa simba wao wameshupalia hill tu! Huu ni utoto wa kutamani baba amiliki ghorofa wakati huo uwezo haupo! Kama hatuna taarifa za kutosha kutoka kwa viongozi wetu wakuu tuwe tunaacha kujifariji na kuanza kuwachanganya watu.
Dirisha la usajili linafungwa hakuna taarifa kutoka uongozi wa juu kuwa wamesajili lakini ninyi mmekalia mitandaoni kujifariji tu eti mmemsajili Fulani na fulani! Huu ni ujinga wa kiwango cha juu. Narudia tena, mashabiki wa simba acheni utoto, ongeeni masuala ambayo yana tija kwa ajili ya kuendeleza timu yetu na siyo porojo za vijiweni tu