Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Bila shaka Wanalunyasi mtakuwa mnatamani kupata kiongozi kijana ambaye ana maoni makubwa juu ya klabu yenu kama ambavyo Yanga wamewatesa misimu hii minne mfululizo baada ya Engineer Hersi Said kuchukua kijiti cha Rais wa Klabu baada ya Mshindo Msolla.
Mnahitaji uongozi wenye maono, uwezo wa kifedha, na mtandao mpana wa biashara — sifa ambazo zinaonekana wazi kwa Joseph Rwegasira. Ameonyesha kwa vitendo kuwa ana nia ya dhati ya kuisaidia Simba kupitia uwekezaji, ubunifu wa kibiashara, na ushirikiano na wadau mbalimbali.
Joseph Rwegasira (Jayrutty) tayari ameanza kuijenga Simba bora tangu siku ambayo alisaini mkataba wa Tsh. Bilioni 38 kupitia Kampuni yake ya JAYRUTTY ambaye ni mzabuni wa utengenezaji Jezi, mkataba ambao ulikuwa na ahadi nyingi nzuri ambazo baadhi ameanza kuzitekeleza.