Mashabiki wa Simba bila pressure aibu zaidi inakuja

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kiwango cha Simba kinazidi kuporomoka mno. Mbaya zaidi ni kama wanachama na mashabiki tumekubaliana na hii hali. Tunapaswa kuhoji viongozi wetu, huu ni muda wa uwajibikaji.

1) Kwanini Chama hachezi? Wanaficha nini?
2) Issue ya Morrison ni dhahiri imekaa kihuni hatuambiwi ukweli
3) Kwanini tumejaza professionals ambao hawatumiki?
4) Kwanini morali ya timu ipo chini sana?

Ni muhimu tuamke tudai mabadiliko sasa bila kujali msimu upo hatua gani. Timu inacheza ovyo mfululizo na hakuna hatua za msingi kuleta mabadiliko. Tumewapa Yanga ubingwa kijinga!

Viongozi wetu hawafanyi kazi bila pressure, tumevumilia inatosha! Tujue hatma ya timu sasa!
 
Subirini mechi na Uto kwanza,mkianza kuvutana muda huu, msije kumlaumu mtu na kusema hamkuambiwa.
 
Shida ni Pablo,
 
1.Kule kufukuza makocha hovyo kulisababisha kila kocha anayekuja aje na mbinu zake, tena mbaya zaidi wanafukuza katikati ya msimu.

Hii ilisababisha kuirudisha timu nyuma, viongozi walijiamini sana Simba lazima iwe bingwa no matter what, matokeo yake ndio haya wamefunguliwa macho.

2. Kuhusu Morisson kwangu simuhitaji, yule jamaa ni kirusi, mpira anao lakini discipline hana, hili ni tatizo ambalo haliwezi kuvumiliwa muda mrefu lingeigarimu timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…