Mashabiki wa Simba mnaonaje Sakho auzwe?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Hizo offer zinazotolewa ni kubwa mno, zaidi hata ya Luis Miquison!

Je unaonaje auzwe halafu Miquison arudi au aletwe mzuri zaidi.

Maana Sakho hata hivyo ana mapungufu mengi tu pamoja na kuwa na goli bora Afrika.
 
Auzwee, waletwe wengine wakiwemo Manzoki na Okwaa.

Miquisson hawezi kubali, mtonyo ni mrefuuu. Tuwatafute players wengineee.
 
Hizo offer zinazotolewa ni kubwa mno ,zaidi hata ya Luis Miquison!

Je unaonaje auzwe halafu Miquison arudi au aletwe mzuri zaidi.

Maana Sakho hata hivo ana mapungufu mengi tu pamoja na kuwa na goli bora Africa.
Mchezaji kuuzwa au kununuliwa haiko ndani ya uwezo wa mashabiki. Timu inayojiendesha kibiashara hununua wachezaji na kuuza wachezaji kwa wakati sahihi. Simba inasajili wachezaji wenye umri mdogo kwa kuzingatia hili na kuzingatia pia malengo ya timu.

Utopolo wao wanasajili kwa maoni ya washabiki. Wamesajili wachezaji 4 wa kigeni na hawajauza hata mchezaji mmoja. Na hata wachezaji waliowasajili hakuna hata mmoja atakayeuzika baada ya msimu mmoja kuisha.

Wamewacha kina Ushindinkwa kuwa tu mashabiki wamepiga kelele ila kiuhalisia Ushindi ni mchezaji mzuri sana.
 
Hizo offer zinazotolewa ni kubwa mno ,zaidi hata ya Luis Miquison!

Je unaonaje auzwe halafu Miquison arudi au aletwe mzuri zaidi.

Maana Sakho hata hivo ana mapungufu mengi tu pamoja na kuwa na goli bora Africa.
Kwanza lazima mjue sisi wapenzi tunaona pengo la Luis halijawahi kuzibwa.Huyu Sakho angalau alifanya timu iwaweke roho juu mabeki wa timu pinzani.Watu wasumbufu kwa mabeki kama Morrison mmepata?
Vinginevyo itakuwa ni ujinga ule ule mliofanya mwaka jana.
Je mnadhani Yanga hawajapewa ofa kubwa kwa Mayele?
Kwa nini hawajamuuza?Tuacheni tamaa ya pesa
 
Binafsi naamini msimu ujao ana nafasi ya kuongeza thamani yake zaidi sababu sasa hivi agents wengi wanamtazama baada ya goli bora kuwaamsha.

Kama ni kuuzwa auzwe msimu ujao, anaweza leta faida uwanjani katika huo msimu na kifedha ofa zikawa zaidi ya sasa. Ila kama dau zitaenda beyond expectations kwa kiwango cha kushindwa kusubiri, ni sawa pia.
 
Hii dunia sio fair,Sakho goli moja tu la kideo dunia nzima hadi CNN na BBC.mastaa wote wa afrika wanataka kupiga nae picha,Agents dunia nzima wanamtafuta na kutoa ofa.
Yule wa bao 14 katafutwa na timu moja tu ya S.Africa
 
Means yanga wamesajili wastaafu
 
Auzwe haraka kabla ajapata pancha kwanza keshaonyesha ni mtu wa majeraha mara kwa mara alafu anapenda kucheza na jukwaa pasipo na sababu.
 
Hii dunia sio fair,Sakho goli moja tu la kideo dunia nzima hadi CNN na BBC.mastaa wote wa afrika wanataka kupiga nae picha,Agents dunia nzima wanamtafuta na kutoa ofa.
Yule wa bao 14 katafutwa na timu moja tu ya S.Afric
 
Kwaiyo Mane kumbe aliomba picha 🤣🤣
 
Je kiwango kikishuka?? Ligi ya Bongo huijui vizuri eeeh??
Hapa hapa, auzwee tupate pesa tulete wengine.
 
Huyu sakho ana nini cha ajabu?
Hebu tuambieni ana goli ngapi kwenye ligi ya NBC?
Simba acheni vigeugeu kuna kipindi kati hapa kwenye ligi mlipaza sauti waondolewe yeye na wenzake kina banda.

Huyu sakho ambaye kwenye dearby ya kariakoo huwa mnamtoa akakalie bench leo amekua messi?
Sioni tofauti yake na Kibu

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Auzwe tu.
Stamina yake ni ndogo sana pamoja kua anakipaji flani cha mpira.

Kwa uwezo anazidiwa hata na Banda kama atajiamini.
 
Je kiwango kikishuka?? Ligi ya Bongo huijui vizuri eeeh??
Hapa hapa, auzwee tupate pesa tulete wengine.
Unaamini kiwango kinaenda kushuka? Kama unaamini hivyo upo sawa.
 
Ngoja tuone msimu huu unaofuata atapanda thamani au vipi coz kwa umri wake bado ana mengi ya kuifanyia Simba akishirikiana na akina Okrah na Phiri pale mbele.
 
Haya ni maoni tu ya mashabiki ndo maana niliandika maoni ya mashabiki ni nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…