Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Hawa ni changamoto sana.
Timu ikishinda goli chache inatupiwa lawama kuwa kiwango kimeshuka.
Timu ikishinda goli nyingi wale wa upinzani wanasema timu iliyoshinda imenunua mechi na wachezaji.
Timu zao zikishindwa wanatokwa maneno hatari. Wiki nzima mtu atalaumu hatari. Kila mtu anajifanya kocha na mchambuzi wa soka.
Hawa ndugu hawaeleweki kabisa..
Hawana uvumilivu
Wepesi wa lawama
Kila mtu mjuaji
Wanawasema wachezaji wao vibaya kwa maneno ya kukatisha Tamaaa.
Jamani, kama hata Mungu anapewa changamoto na Shetani ije kuwa wanadamu?
Hebu kuweni wavumilivu na muongee kwa staha, acheni kuwatukana wachezaji, makocha na wadhamini wa timu.
Mara mchezaji huyu kanunuliwa, kahongwa sijui imekuwaje....yaani maneno ya dhihaka yasiyokuwa na ushahidi. Wakati performance ya mtu huwa inabadilika kutokana na hali. Mchezaji kajitahidi kucheza vizuri mechi 4 ila akikosea kidogo mechi ya 5 atazodolewa mpaka basi. Mnatia aibu sana katika dunia ya kistaarabu. Nyinyi huko mliko mnafanya mambo yenu vizuri kila siku? Mnakera sana..
Hao wadhamini mnaowarushia maneno ndo wamesaidia kwa pesa zao mpaka leo hii ligi yetu inakuwa miongoni mwa ligi bora Afrika.
Hivi kama isingekuwa hao wadhamini mnaowatukana kutwa nzima kuwa wanafanya hiki na kile, hizo timu ndogo zingepata hata nauli ya kusafiri kila siku? Wachezaji wangelala sehemu nzuri? Kuna timu zingekuwa zinalala kwenye mabweni ya wanafunzi.
Hebu kuweni wastaarabu basi. Mnaboa sana.