Mashabiki wa Simba SC jitokezeni tumsaidie Haji S Manara.

Kwani shoots on target bila goli zina maana gani? Nikiwatazama yanga na jezi zao naona kama mikungu ya ndizi zilizoiva
 
Kwani hujui kuwa Manara naye ni miongoni mwa matatizo ndani ya Simba? Huyu ni wakupuuza tu kwani haya anayoyasema kuhusu Yanga ameanza kusema hivyohivyo tangu msimu wa 2013/2014 ika matokeo ya maneno yake umeyaona.
Miongoni mwa vitu ambavyo Simba inatakiwa kutovionea aibu kabisa ni pamoja na kumuwekea Manara mipaka, huyu ndio mchonganishi mkubwa baina ya uongozi na wanachama, kwani yeye anapambana na Yanga tu wakati Yanga hawapambani na yeye tu na mwisho wa ligi anawaaminisha mashabiki kuwa wanaonewa.
Hata hili la timu ya bilioni 1.3 ni kosa kwa Manara kulishadadia akiona ni sifa bila kujua mazingira ya nchi yenyewe timu ipo, kuna wachezaji wachache sana wanaoifanya hiyo bilioni 1.3 itimie kwahiyo bila kujijua anachochea hasira za wachezaji wengi ambao ni msaada kwa timu pia.
 
Yule mwarabu Mo atamshikisha ukuta mtu huu msimu haiwezekeni libiloni lizima likatoe sare ya kizembe vile na wale vyura wanaonuka njaa mpk unyayoni
Tena Sare yenyewe ya kushukuru Mungu kwani ilikiua Yanga watoke kifua mbele.
 
Yule mwarabu Mo atamshikisha ukuta mtu huu msimu haiwezekeni libiloni lizima likatoe sare ya kizembe vile na wale vyura wanaonuka njaa mpk unyayoni
Duh “wanaonuka njaa mpaka unyayoni”
Dem boy wee ni mchochezi
 
Yanga mbn mnakua wapuuzi mbona nyie mnakuaga na kikosi cha hela kibao na uwa mnafungwa na simba simba ikiwa na kikosi cha watoto chirwa alisajiliwa kwa sh ngap au mmesahau au mnakariri kwamba usajili ni msimu mmoja
 
Kwani shoots on target bila goli zina maana gani? Nikiwatazama yanga na jezi zao naona kama mikungu ya ndizi zilizoiva
Unaziona hivyo hizo jezi kwa sababu una makengeza ya moyo. Ndio maana huoni maana ya ‘shoots on target.’
 
Yanga mbn mnakua wapuuzi mbona nyie mnakuaga na kikosi cha hela kibao
Povu la nini Boss!

Yanga anapokuwa kwenye ubora wake kifedhwa huwa mpaka muda huu anakuwa anaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 5 na sio mabao tu.
 
chirwa alisajiliwa kwa sh ngap au mmesahau au mnakariri kwamba usajili ni msimu mmoja


Hata zikijumlishwa gharama za Yanga za usajilikwa misimu 2 yaani 2016/17 na 2017/18 bado hazifiki kiasi cha Bilioni 1.3
 
Yanga Aka 'Wanga' kandambili original wanafuraha iliyopitiliza kuchoropoka mdomoni mwa mnyama.
Sio kwa furaha hii jamani! Sare mnaifurahia namna hii!!?


Unajiitaje simba kama mnyama swala amekuchoropokamdomoni mwako mara 2 mfululizo...?

Kumbuka kuwa kuna simba wa kufungwa, huwa wanakula kiepe yainao.
 
Vyura fc wamezoea kufungwa kila siku na mmewao simba,sasa wanashangilia sare.aya ongereni kwa ushindi wa jana
Unazungumza kila siku...?

Hebu tafuta jumla ya mechi za simba na yanga then angalia nani aliyekuwa anamfunga mwenzake kila siku..

Bila shaka anayemfunga mwenzake kila siku atakuwa ni yule ambaye amemfunga mwenzake jumla ya games nyingi.
 
Simba kila mwaka anaanza kuwa Simba lkn mwishoni anakuwa paka.Hivyo Wanayanga wasihofu Simba tayari anaelekea kibra kama kawa!

Evolution ya Simba ni hivyo hivyo... Mwanzoni mwa Ligi anakuwa simba.

Mwishoni anakuwa paka...na kufikia kuwa Nyau...na ligi ikiisha anakuwa NYUMBU wa kudai alama za timu nyenginezo.
 
Kwani mbona misimu 2 iliyopita timu yenu ilikuwa ikisajili kwa gharama kubwa kuliko Simba SC lakini mlishindwa kupata ushindi zaidi tu Kichuyaaaaa akipeleka maangamizi, je mlikumbwa na nini kifafa au?

Hongera kwa ushindi wa jana . sare kwenu ushindi
 
Matopeni Fc tabu kwelikweli wamebaki wanaduwaaa Kikosi cha 1.3B hamna kitu
 
Na mwisho wa ligi ndio bingwa....simba aliyewaroga naomba awasamehee jaman.
 
Hahahaaa pesa za mafisango za rambirambi walizokula mpk warudishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…