NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 11,297
- 14,588
Katika hali ya kushangaza lakini ya kweli, mashabiki wa Simba SC wamekuwa kama mkia wa kondoo wanajikaanga wenyewe bila hata ya kuhitaji moto wa nje. Timu yao imekuwa ikipitia misimu ya maumivu: kushindwa kwa mipango ya usajili, kukosekana kwa mwelekeo wa kiufundi, na viongozi wanaozunguka mduara bila suluhisho , lakini bado mashabiki wanashabikia kwa macho mafupi kana kwamba kila kitu kiko sawa.
Cha kusikitisha zaidi, badala ya mashabiki kuungana na kuwa sauti ya pamoja ya mabadiliko, sasa wamegawanyika kama vyama vya siasa. Wamekuwa watu wa kutupiana vijembe mitandaoni na makundi ya mashabiki, kila mmoja akimtetea kiongozi anayempenda badala ya kuangalia maslahi ya timu kwa ujumla. Hakuna mshikamano, hakuna hoja za msingi ni kelele, vijembe, na visasi.
Mbaya zaidi, kuna baadhi ya mashabiki wanaolipwa na viongozi wa klabu ili kuwasafisha hadharani na kuwashambulia wale wote wanaokosoa. Hawa wamegeuzwa kama askari wa propaganda, wakijifanya wana mapenzi na klabu lakini kiuhalisia ni vibaraka wanaotumiwa kuficha uozo unaoendelea. Kwao, kila kitu kiko sawa mradi pochi inatetemeka. Wamesahau kabisa wajibu wao wa msingi wa kuhoji, kushauri na kulinda heshima ya timu yao.
Kwa sasa, mashabiki wa Simba SC wamefikia hatua ya kubishana wao kwa wao bila kujua adui yao wa kweli ni uzembe ndani ya klabu yao. Ligi ikianza tu, na mpinzani wao mkubwa Yanga SC akianza kushinda, kelele zinaanza: “GSM amenunua mechi,” “GSM anadhamini timu nyingi, ndiyo maana wanapewa pointi kirahisi.” Hii ni dalili ya kushindwa kujitathmini na kukubali ukweli kuwa Simba SC kwa sasa haina ubora wa kuhimili ushindani.
Kwenye uongozi wa Simba SC kuna madudu makubwa sana. Uongozi umekuwa wa kizamani, wa mazoea, usio na dira wala uwazi. Kama hakutapatikana uwajibikaji wa kweli wa viongozi kuhojiwa, kushinikizwa na hata kujiuzulu inapobidi , basi tutaendelea kushuhudia kilio cha mara kwa mara kwa mashabiki wa Simba SC. Zaidi ya hapo, tutaona pia hadhi ya Kariakoo Derby ikishuka taratibu kwani haitakuwa tena vita ya wababe wawili, bali pambano la upande mmoja na timu isiyo na mpango.
NALIA NGWENA, nimekuwa mshauri mkubwa sana katika hili kupitia jukwaa pendwa la michezo hapa Jamii Forums. Nimeandika, nimekosoa kwa hoja, nimetahadharisha lakini utekelezaji umekuwa sifuri. Viongozi wanafunga masikio yao, na mashabiki wanachezewa kihisia kila msimu kwa ahadi tamu zisizo na utekelezaji. Wanaburuzwa kama watoto, huku heshima ya klabu yao ikiporomoka kwa kasi ya kutisha.
Kwa kifupi, mashabiki wa Simba SC wanapaswa kuamka. Kuendelea kuwabeba viongozi kwa makosa yao ni sawa na kujiangamiza taratibu kama mkia wa kondoo unaojiangusha kwenye sufuria ya moto, Wakati umefika wa kusema “hapana,” kudai mabadiliko ya msingi, na kuitaka Simba irudi kwenye hadhi yake kama klabu ya ushindani, heshima, na historia kubwa barani Afrika
TUENDELEE KULA MTORI NYAMA TUTAZIKUTA CHINI
View: https://youtu.be/Rw5glyqwj0U
View: https://youtu.be/CDJofTTZfoY?si=RJOzvNjKNO_nORPl